RAIS MAGUFULI AWAKUTANISHA DIAMOND PLATINUMZ NA ALI KIBA DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 13 July 2020

RAIS MAGUFULI AWAKUTANISHA DIAMOND PLATINUMZ NA ALI KIBA DODOMA

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli jijini Dodoma akisalimiana na msanii Ali Kiba (kushoto) Ikulu ya Chamwino katika hafla ya chakula cha pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli jijini Dodoma akisalimiana na msanii Diamond Platinumz (kushoto) Ikulu ya Chamwino katika hafla ya chakula cha pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo.

Wasanii Ali Kiba (wa tatu kushoto) pamoja na Diamond (wa pili kulia) wakiwa Ikulu ya Chamwino katika hafla ya chakula cha pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na wageni waalikwa.

Wasanii Diamond na Mwenzake Ali Kiba na wasanii wenginea wakifurahiya jambo Ikulu ya Chamwino katika hafla ya chakula cha pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo.
  
Msanii nguli Ali Kiba (jukwaani) akitumbuiza wageni katika Ikulu ya Chamwino kwenye hafla ya chakula cha pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo.

Msanii Diamond akiwatumbuiza wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo jana.

Wasanii anuai pamoja na Kiba na Diamond katika picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa CCM na Rais JPM.

Msanii Diamond (kulia) akionesha mambo ni dole pamoja na JPM aliyewakutanisha Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Wakifurahiya jambo kwa pamoja.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

UNAWEZA kusema wasanii maarufu nchini Diamond Platinumz pamoja na mwenzake Ali Kiba wamemaliza bifu zao zilizodumu kwa muda mrefu baada ya kukutanishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli jijini Dodoma.

Tangu juzi mjini hapa kiongozi huyo, JPM ambaye kwa sasa atapeperusha tena bendera ya CCM kugombea nafasi ya urais aliwaalika wasanii hao na wengine katika mkutano mkuu wa CCM na baadaye ikulu ya Chamwino pamoja na wajumbe wengine wa mkutano huo kwa chakula cha pamoja.

Wasanii Diamond pamoja na Kiba walijikuta wanakaa meza moja huku wakisahau tofauti zao na kucheka pamoja, kufurahia mwaliko huo wa JPM viwanja vya Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Katika hafla hiyo Diamond alitumbuiza pamoja na Kiba jukwaa moja kwa furaha na kusahau kabisa tofauti zao (mabifu yao), na kupiga picha ya pamoja na mwenzake wakiwa na Rais JPM na wasanii wengine ikiwa ni kumbukumbu ya tukio hilo la kihistoria.

Msanii Diamond Platinumz alitumbuiza wimbo wake pendwa "Magufuli Baba Lao" wakati mwenzake Ali Kiba akikonga nyoyo za wageni mbalimbali na kulipua shangwe jukwaani akitumbuiza.

Muunganiko huu huenda ukamaliza kabisa bifu la manguli hawa wa muziki wa kizazi kipya lililodumu miaka kadhaa huko nyuma huku mara zote wakitupiana vijembe kila mmoja wao.

No comments:

Post a Comment