MAKADA 460 KAGERA WAJITOKEZA KUWANIA UBUNGE CCM, BUKOBA MJINI YAONGOZA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 17 July 2020

MAKADA 460 KAGERA WAJITOKEZA KUWANIA UBUNGE CCM, BUKOBA MJINI YAONGOZA

Watia nia wa Jimbo la Bukoba mjini wakiwa katika kikao na viongozi wa wilaya baada ya kurejesha fomu za kuwania kuteuliwa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Kagera, Machael Chonya akitoa taarifa ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania kuteuliwa nafasi za ubunge kwa vyombo vya habari ofisini kwake.
Na Allawi Kaboyo, Bukoba
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 460 wachukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge wa majimbo pamoja na viti maalumu mkoa wa Kagera.
Akiongea mjini Bukoba na waandishi wa habari katibu wa CCM Mkoa wa Kagera, Ndg. Michael Chonya amewaeleza waandishi wa habari kuwa mwenendo wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuomba uteuzi ndani ya chama chao kwa ngazi zote umekwenda vizuri kwa kujitokeza wananchama wengi kuomba kuteuliwa.
Chonya ameeleza kuwa wanachama walioomba kuteuliwa ngazi ya ubunge wa majimbo ni 404 na waliojitokeza kuomba kuteuliwa ngazi za ubunge wa viti maalumu ni 56 kwa mkoa mzima.
“Katika mkoa wetu wa Kagera wanachama waliotia nia kuomba kuteuliwa wapo 460 ambao wamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni ubunge wa majimbo ni 404 na upande wa jumuia za vijana na wanawake ambao jumla yao ni 56 na mchakato tumeufunga leo tarehe 17 julai 2020 saa kumi kamili jioni.” Ameeleza Chonya.
Chonya amefafanua kuwa katika majimbo tisa ya uchaguzi yaliyopo mkoani Kagera wanachama waliojitokeza kuchukua na kurejesha fomu kwenye majimbo ya Bukoba mjini ni 57, Bukoba vijijini 42, Muleba kasikazini 17, Muleba kusini 52, Biharamulo 51, Ngara 43, Kyerwa 52 Karagwe 36 na jimbo la Nkenge wanachama 54 ambao jumla yao wanaleta wanachama 404.
Ameongeza kuwa kwa upande wa ubunge viti maalumu wanawake UWT ni Wanachama 34, Vijana UVCCM 19 na Jumuiya ya wazazi 3 ambao jumla yao ni wanachama 56 ambao wanaufanya mkoa huo kuwa na wagombea 460 kwa nafasi ya ubunge.
Aidha ameongeza kuwa baada ya mchakato mzima wa kuchukua na kurejesha fomu sasa mchakato unaofata ni mikutano ya kupiga kura za maoni kwa wilaya pamoja na mabaraza ya jumuiya ili kuweza kuwapata wagombea watakao pelekwa kwenye vikao kwaajili ya teuzi.
Chonya amewasihi watia nia hao kuendelea kuwa watulivu na kuepuka kuvunja sharia na kanuni za chama katika kipindi hiki ambacho chama kinaendelea na mchakato ili kuepuka viashiria vya uvunjifu wa nkanuni.

No comments:

Post a Comment