JPM ASHINDA KWA KISHINDO KUPEPERUSHA BENDERA YA URAIS CCM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 11 July 2020

JPM ASHINDA KWA KISHINDO KUPEPERUSHA BENDERA YA URAIS CCM

Dk. John Pombe Magufuli.

MKUTANO Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo umemchagua rasmi Dk. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa mkutano wa uchaguzi katika kikao hicho akitangaza matokeo alisema Dk. Magufuli amepata kura 1,822 kati ya kura zote 1822 za wajumbe waliohudhuria mkutano huo.

bacho ni chama tawala nchini Tanzania, imemchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk. Hussein Mwinyi kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Serikari ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupitia CCM Zanzibar.

Waziri Mwinyi ameibuka mshindi bajada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili. Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika jijini Dodoma umehudhuliwa na wajumbe na wageni mbalimbali takribani 2000 kutoka nje na ndani ya nchi.

No comments:

Post a Comment