Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiwashukuru wajumbe mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni wakati wa mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe, Leo Tarehe 20 Julai 2020. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akionyesha kitabu cha utekelezaji wa ilani katika kipindi cha miaka mitano 2015-2020 wakati wa kura za maoni kwenye mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe, Leo Tarehe 20 Julai 2020.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiwashukuru wajumbe mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni wakati wa mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe, Leo Tarehe 20 Julai 2020.
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiwa amemaliza kuhesabu kura alizopata kabla ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni wakati wa mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe, Leo Tarehe 20 Julai 2020.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga ameibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni wakati wa mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe.
Hasunga ameibuka mshindi baada ya kuwamwaga wapinzani wake kwa ushindi wa kura 552 sawa na asilimia 76.4.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mhe John Palingo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi amesema kuwa idadi ya wajumbe wa mkutano huo ni 801 lakini wajumbe waliopiga kura ni 736 huku kura 13 zikiwa zimeharibika.
Palingo amemtaja Erick Minga aliyepata kura 129 kuwa ndiye aliyeshika nafasi ya pili akifuatiwa na wagombea wengine ambao ni Dismas Haonga- 9, Alex Edward - 7, Augustino Simbeye- 7, Denis Simbeye-1, Faraja Mwambalo- 2, George Ambilikile-3, Jerald Silwimba-0, Jumanne Sichinzya-3, Oscar Magwaza-1, Stanislaus Nsojo- 3, Stephen Mwamengo-1, Christopher Mwawalo- 3, na Chrispin Mwashambwa-0
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Vwawa, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amewashukuru wajumbe kwa kumuamini huku akiwapongeza washindani wake na akisisitiza ulazima wa wagombea wote kuungana pamoja ili kuhakikisha kuwa CCM inashinda uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu.
Amewasihi wagombea wenzanke kutotengeneza makundi mara baada ya uchaguzi kumalizika badala yake amewataka kuungana pamoja ili kukipigania Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuwasihi kutotumia lugha za kuuzi mara baada ya kushindwa.
Kwa upande wake wagombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo hilo Bw Erick Minga, Stanslaus Nsojo na Dismas Haonga wamesema wameunga mkono matokeo yaliyotangazwa huku wakisisitiza kuungana na atakayeteuliwa na chama kupeperusha bendera ya CCM ili kuhakikisha inashinda uchaguzi mkuu ambapo pamoja na mambo mengine wamempongeza mshindi wa uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment