BILIONEA LAIZER AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA GePG - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Sunday, 12 July 2020

BILIONEA LAIZER AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA GePG

Bilionea mpya nchini Tanzania ambae ni Mchimbaji wa Madini Bw. Saniniu Laizer, akisaini daftari la wageni wakati alipofika kutembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Afisa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda akimuonesha Bw. Saniniu Lazier, mfumo wa kielektroniki unaoonesha muenendo wa makusanyo ya Serikali kwa Taasisi zote za kwa kila siku ikiwa ni njia ya kuongeza uwazi na kudhibiti makusanyo ya fedha za umma, wakati alipotembelea banda la Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Ramadhani Kissimba (kushoto) akimuongoza Bw. Saniniu Laizer, kutembelea banda la Wizara pamoja na Taasisi zake wakati alipotembelea banda hilo kujionea huduma na elimu inayotolewa kwa umma wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment