BALOZI WA UJERUMANI AMSIFU JPM KUKUZA UCHUMI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 11 July 2020

BALOZI WA UJERUMANI AMSIFU JPM KUKUZA UCHUMI

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, (wa tatu kushoto) akiwaongoza wawakilishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kumkaribisha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, alipofika kujionea huduma na elimu inayotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda, kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) wenye lengo la kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment