Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza. |
KWA MUJIBU wa taarifa ya Msemaji wa Serikali ya Burundi, Balozi Willy Nyamitwe, Rais Pierre Nkurunziza mwenye umri wa miaka 55 amefariki kwa mshtuko wa moyo kinyume na uvumi unaoenezwa.
Serikali ya Burundi imetangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza, katika ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa Twitter, unaosema kwamba Agosti 8 "Timu ya madaktari walishindwa kunusuru maisha yake baada ya kupata mshutuko wa moyo."
Serikali ya Burundi imetangaza siku saba za maombolezo na ametuma salamu za ramirambi kwa familia. Serikali inasema kuwa alilazwa hospitalini Jumamosi iliyopita.
Jumamosi, Bwana Nkurunziza, ambaye anapenda sana masuala ya michezo, alikuwa anahudhuria mashindano ya voliboli, katika uwanja ulio karibu na nyumbani eneo la Buye, mkoa wa Ngozi kaskazini mwa Burundi kabla ya kukimbizwa hospitali ya karusi katika mwa nchi hiyo jioni.
Bwana Mr Nkurunziza, baba ya watoto watano amega dunia huku mke wake Denise Nkurunziza akiwa anatibiwa kwa ugonjwa usiojulikana mjini Nairobi, nchini Kenya tangu Mei 28, afisa katika ofisi ya rais amezungumza na idhaa ya BBC ya Maziwa Makuu.
Bado haijafahamika ikiwa Bwana Nkurunziza alikuwa na virusi vya corona wakati anapata matibabu. Serikali ya Burundi imeripoti visa 83 vya walioathirika na corona lakini pia hatua za Shirika la Afya Dunia za kukabiliana na virusi vya corona hazikuchukuliwa wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi huo.
Pierre Nkurunzizaamekuwa mwanasiasa wa Burundi na kuwa madarakani tangu mwaka 2005. Bwana Nkurunziza, kijana wa aliyekuwa mbunge, alinusurika mauaji 1993 ya wanafunzi wa Kihutu katika chuo kiuu cha Burundi ambapo alikuwa mhadhiri na kujiunga na waasi wa FDD kundi ambalo baadae lilibadilika na kuwa chama tawala cha CNDD-FDD ambacho alikuja akawa kiongozi.
Alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD-FDD, hadi alipochaguliwa kama rais wa Burundi. Baada ya makubaliano ya Amani ya Arusha kati ya serikali na waasi, Nkurunziza alitajwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kabla ya bunge kumchagua kama rais Agosti 2005.
2015, Nkurunziza alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa na utata na chama chake kwa muhula wa tatu madarakani. Wafuasi wake na wanaompinga Nkurunziza walikosa kukubaliana katika suala la ikiwa ilikuwa halali kwake kugombea tena na maandamano yakafuata.
Zaidi ya miezi miwili kulitokea maandamano ya kumpinga Nkurunziza ambayo yaliandamana na ghasia na kusababisha vifo vya watu. Mei 13, 2015, jaribio la mapinduzi dhidi ya Nkurunziza lilitokea akiwa nje ya nchi hiyo.
Mkuu wa mapinduzi hayo Jenerali Godefroid Niyombare alidai kwamba amemng'oa mamlakani Nkurunziza lakini wanajeshi watiifu kwa Nkurunziza walikanusha madai hayo.
Nkurunziza ameongoza taifa hilo kwa miaka 15.
Rais Pierre Nkurunziza aliyezaliwa Desemba 18, 1963 alikuwa ameratibiwa kumkabidhi mrithi wake madaraka jenerali Evariste Ndayishimiye. Burundi ndio tu imekamilisha uchaguzi mkuu mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi ya Burundi, katika uchaguzi uliofanyika Mei mwaka huu mgombea wa chama tawala cha Everiste Ndayishimye ndiye aliyetambuliwa kuibuka na ushindi. Hivyo basi, Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alitakiwa kumkabidhi madaraka.
Evariste Ndayishimiye, rais mteule amepangiwa kuapishwa Augosti 20 kumrithi Nkurunziza ambaye amekuwa akiongoza taifa hilo tangu 2005 yaani miaka 15. Ndayishimiye ni mwanasiasa wa karibu wa Nkurunziza na amekuwa Katibu Mkuu wa Chama tawala cha CNDD-FDD tangu mwaka 2016.
Alizaliwa mwaka wa 1968 katika mkoa wa Gitega, eneo la kati mwa taifa hilo.
-BBC
No comments:
Post a Comment