Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi akizungumza wakati akitoa elimu katika semina ya siku mbili inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga.
AFISA wa Tathimini na Ufuatiliaji wa Taasisi ya TEWOREC akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Majira Mashaka Mhando akitoa uzoefu wake wakati wa semina hiyo.
Akizungumza kwenye semina ya siku mbili inayotolewa kwa Wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegals) kutoka halmashauri 11 zilizopo mkoani Tanga, Kaimu Ofisa Afya wa Jiji la Tanga Hamza Maulidi alisema wananchi hawana budi kumpongeza Rais kutoka na kututoa hofu tangu alipogundulika mgonjwa mmoja hapa nchini.
Alisema kweli ugonjwa huo bado upo nchini na wananchi waendelee kuchukua tahadhari zote pamoja na kwamba maambukizi yanashuka kwa kasi kubwa Jijini hapa, lakini pia wanampongeza Rais kwa hatua alizochukua hadi ugonjwa unaendelea kupungua.
"Ugonjwa upo na Tanga pia upo, tuchukue hatua tunazoelekezwa na wataalamu wetu wa afya, lakini kwa kweli tunampongeza mheshimiwa Rais kwa kututia faraja tangu ugonjwa huu umeanza," alisema Maulidi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walisema yametolewa wakati muafaka ambao shughuli za kiserikali nyingi zimeanza kufanyika baada ya mikusanyiko kuzuia hivyo itawasaidia kupata uelewa mkubwa wa ugonjwa huo na taadhari zake.
Awali akifungua mafunzo hayo Meneja wa Shirika la kutoa msaada wa kisheria mkoani Tanga (TAWOREC) Halima Saguti alisema lengo la kutoa mafunzo kwa Paralegal hao ni kutaka wanapotoa huduma kwa wananchi huko vijijini waweze kujiinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Alisema kazi za wasaidizi hao wa kisheria zimekuwa zikiendelea huko vijijini na hivyo kupewa elimu hiyo kutasaidia kupunguza kusambaa kwa ugonjwa huo kwa watu wengine.
No comments:
Post a Comment