WATU 18 WAMEFARIKI NA WENGINE 15 KUJERUHIWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 15 April 2020

WATU 18 WAMEFARIKI NA WENGINE 15 KUJERUHIWA

Eneo ilipotokea ajali


WATU 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Kamanda Lyanga amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Aprili 15, 2020 na kwamba imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amebainisha Lyanga.

Amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

Kamanda Lyanga amesema majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.

No comments:

Post a Comment