Waziri wa Afya Ummy Mwalimu |
WAGONJWA wapya 29 wathibitishwa kuwa na virusi vya corona katika mji wa Dar es Salaam nchini Tanzania. Idadi hiyo inafikisha watu 88 walioambukizwa na Covid 19 kufikia sasa.
Kulingana na taarifa ya wizara ya Afya, wagonjwa 26 kati yao wapo katika mji wa Dar es Salaam huko wawili wakipatikana mjini Mwanza na mmoja akiwa katika eneo la Kilimanjaro.
Waziri wa Afya Ummi Mwalimu anasema kwamba ufuatilianaji wa watu waliokaribiana na wagonjwa haoo unaendelea.
Hatahivyo waziri huyo ametangaza habari njema akisema kwamba hadi kufikia leo Jumatano takriban watu 11 wamepona virusi hivyo lakini akaongezea kwamba watu wanne walifariki.
Ongezeko hilo la wagonjwa linajumlisha wagonjwa wapya sita waliotangazwa na waziri wa Afya wa kisiwa cha Zanzibar.
Serikali hatahivyo imewasisitizia wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment