RC HAPI:BENKI YA TOFARI MKOMBOZI WA MAJENGO MAPYA IRINGA. - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 2 March 2020

RC HAPI:BENKI YA TOFARI MKOMBOZI WA MAJENGO MAPYA IRINGA.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akitoa maelezo ya namna gani ya kuzipata tofali kwa ajili ya kuhifadhi kwenye kila kijiji au mtaa.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
MKUU wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amewataka viongozi wote wa vijiji na mitaa katika mkoa wa Iringa kuhakikisha wanakuwa na benki ya Tofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na majengo ya serikali pale yanapo hitajika.

Akiwa katika ziara ya Iringa mpya awamu ya pili kutokana na uchakavu wa majengo mengi ya shule za msingi na vyumba vya madarasa,nyumba za wafanyakazi wa kada mbalimbali wa serikali katika maeneo husika kuna haja ya kuweka mkakati wa kuanzisha benk ya tofali ili kuboresha na kuanzisha majengo mapya katika maeneo husika.

“Naagiza viongozi wote kuhakikisha wanasimamia wananchi kufyatua tofali za kutosha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo mbalimbali katika vijiji au mitaa husika pale panapo hitajika” alisema Hapi

Alisema kuwa umuhimu wa benki ya tofali na pale inapotokea kuna upungufu wa majengo kwa ajili ya matumizi ya kiserikali inakuwa kazi rahisi kuanzisha ujenzi wa majengo au jingo husika kwa kuwa tayari tofali zipo.

Aidha Hapi aliwaagiza wakurugenzi wote wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanaandika andiko kwa ajili ya kuombe fedha kwaajili ya shule zote zilizojengwa miaka ya 1960 kwa kuwa miundombinu yao kwa sasa haipo vizuri.

Katika ziara yangu nimekugundua kuwa fedha za lipa kulingana na matokeo (EP4R) zimetumika vizuri na kuleta matokeo chanya katika mkoa wetu wa Iringa,kwani majengo mengi yamejengwa kwa viwango vianavyotakiwa.

No comments:

Post a Comment