MENEJA
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
akizungumza na waumini wa kanisa la Adventist (Wasabato) wakati
akihamasisha juu ya vifurusi vipya vya mfuko huo katika halmashauri ya
wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally
Mwakababu kushoto akitoa elimu kwa mfanyabiashara wa viatu wilayani
Kilindi kuhusu umuhimu wa kujiunga na bima ya afya wakati wa uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
AFISA
Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)
Macrina Clemence kulia akiwa na Mhasibu Mwandamizi wa NHIF Tanga
Fredrick Mtangoo wakihamasisha mpango wa bima ya afya kwa wakazi wa mji
wa Songe wilaya ya Kilindi wakati
uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
AFISA
Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga
Josephine John akitoa elimu kwa wananchi wa mji wa Songe wilaya ya
Kilindi wakati
uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
AFISA
Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga
Josephine John akitoa elimu kwa wananchi wa mji wa Songe wilaya ya
Kilindi wakati
uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
AFISA
Metekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)
Macrina Clemence kulia akitoa elimu kwa wafanyabiashara wa soko la Songe
wilayani Kilindi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
AFISA
Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Tanga
Josephine John kushoto akitoa elimu kwa mfanyabiashara kwenye mji wa Songe wilaya ya Kilindi.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani
Tanga (NHIF) umepiga kambi wilayani Kilindi Mkoani Tanga kwa ajili ya zoezi la
uhamasishaji wananchi juu ya vifurushi vipya katika halmashauri ya wilaya hiyo.
Uhamasihaji huo ulifanyika kwenye maeneo
makao makuu ya wilayani hiyo Songwe kwenye maeneo ya kanisani, msikitini,sokoni
,vituo vya bodaboda na stendi ya mabasi lengo kubwa kuwapa uelewa wananchi
umuhimu wa kujiunga na mfuko huo.
Akizungumza wakati wa uhamasishaji huo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
alisema kwamba lengo la kufika wilayani humo ni kuwafikia wananchi na
kuzungumza nao juu ya umuhimu wa mfuko huo.
Alisema kwamba wananchi wengi,wafanyabiashara
ndogondogo ,wananchi wa kawaida
walifikiria bima ya Afya ni kwa ajili ya viongozi,wakubwa na waajiriwa
lakini wao wamefika kuwaeleza kwamba mfuko huo ni kwa ajili ya wananchi wote.
Meneja huyo alisema kwamba hivi sasa
wana fao la Jipimie ambalo wamefika wilayani humo kuzungumza na wananchi katika
maeneo yao ya biashara kuhusu umuhimu wa kujiunga nao.
“Kubwa zaidi wafanyabiashara wanapaswa
kutambua kwamba ili waweze kuendeela na biashara zao ni muhimu kuwa na bima ya
afya watatibiwa wakati wanapoumwa na hawatamaliza mitaji yao kwa sababu gharama
za matibabu hazitawasumbua “Alisema Meneja huyo .
Aidha alisema pia alisema familia wakati
mwengine zimekuwa zikiingia kwenye matitizo wakati mtoto anapoungua,mama hivyo
ni fursa nzuri ya wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanajiunga na bima ya
afya ili waweze kunufaika na matibabu wakati wanapougua.
Akizungumzia mpango huo,Mwenyekiti wa
CCM wilaya ya Kilindi Bakari Kingalangala alisema kwamba mpango wa bima ya afya
ni muhimu sana kwa jamii kwa sababu watu ambao hawana bima ya afya wanapoungua
wanatoa fedha nyingi sana kugharamia matibabu na wakati mwengine kuyumba
kiuchumi.
Alisema lakini wanapokuwa na bima ya
afya inawasaidia kuweza kupata matibabu bila kuwaza kwamba watapata wapi fedha
za kwenda kupata matibabu wanapoungua.
“Bima ya Afya ni muhimu sana kwa jamii
kwa sababu mimi mwenyewe nimewaona watu ambao hawana uwezo wakipata mateso wakifika
vituo vya afya, hospitalini kama huna bima unatoa fedha nyingi sana lakini
ukiwa nayo inakusaidia kutibiwa na unaepuka gharama kubwa”Alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba wayakuwa wahamasishaji kuwaeleza viongozi wa chama
ngazi ya wilaya, kata na vijiji umuhimu
wa kujiunga na mpango wa bima ya afya ili kuweza kunufaika na huduma za
matibabu pindi wanapougua.
No comments:
Post a Comment