SHIRIKA la Afya
Duniani (WHO) limetahadharisha kuwa katazo la kusafiri kudhibiti kuenea kwa
kirusi korona ambacho ni kipya kilichoibuka China linaweza kufeli na kupelekea hali
ya kuenea kwa janga hilo kuwa mbaya zaidi duniani.
Ripoti za hivi karibuni zinaonyesha
idadi iliyothibitishwa ya wagonjwa wenye kirusi hicho kukaribia 12,000, ikiwemo
vifo 259, na wagonjwa wengi kati ya hao na vifo vyote vimetokea China.
Kamati ya masuala ya dharura ya WHO
imetangaza kuwa kirusi corona ni tishio la afya ya umma ulimwenguni Alhamisi,
na kuibua mapendekezo kadhaa yanayo kusudia kupunguza kasi ya kuenea kwa
ugonjwa huo.
WHO haipendekezi kuweka zuio lolote
la kusafiri na biashara pamoja na kuwepo ongezeka la kasi la ugonjwa huo nchini
China na haupungui, lakini unaendelea kuenea ulimwenguni. Zaidi ya watu 100
wameripotiwa kuwa na ugonjwa huo katika nchi nyingine 22.
Ili kukabiliana na hali hiyo, baadhi
ya mashirika ya ndege yamesitisha safari zake kwenda China bara. Marekani,
ambayo imetangaza maambukizo ya kirusi corona kuwa ni dharura ya umma, inasema
itazuia wageni kuingia nchini humo ambao hivi karibuni walikuwa wametembelea
China.
Australia inasema itachukuwa hatua kama za Marekani.
Msemaji wa WHO Christian Lindmeier,
anasema kufunga mipaka hakuwezi kuzuia kirusi hicho kuingia katika nchi
nyingine
“Kama sote tunavyojua katika matukio
mengine ya maambukizi, iwe Ebola au magonjwa mengine, pale watu wanapotaka
kusafiri, watafanya hivyo. Na iwapo njia rasmi za kupita zikiwa zitafungwa,
watapita katika njia za panya,” amesema Lindmeier.
“Lakini njia pekee ya kudhibiti
maambukizo, kupima iwapo mtu ana homa, kwa mfano, kutambua historia ya safari
yake, kujaribu kufuatilia nani anapita katika mpaka wako na kuona iwapo wana
dalili zozote za maambukizo ni kupitia mipaka rasmi.
Lindmeier anasema nchi zinahaki ya
kiutawala kuchukua hatua zozote wanazoamini ni bora katika kuwalinda raia wao
wasipate maambukizo.
“Hata hivyo mapendekezo yatafuatwa.
Na, iwapo katazo la kusafiri litatolewa, tunatarajia kuwa litakuwa la muda
mfupi iwezekanavyo ili watu waweze kuendelea na maisha yao vyema kwa kadiri
itakavyowezekana,” amesema Lindmeier.
“Lakini bila shaka, tuongeze uangalizi
na ufuatiliaji ili kuepuka kuenea kwa ugonjwa huo.”
China inachukuwa hatua kali kuzuia
kuenea kwa kirusi corona. Mji wa Wuhan, ambapo ni chimbuko la ugonjwa huo na
miji mingine 15 imewekewa karantini, na watu takriban milioni 50 wamekatazwa
kutoka nje.
Pamoja na juhudi hizo, kirusi hicho
bado kinaendelea kuenea kwa kasi.
-VOA
No comments:
Post a Comment