TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 12.02.2020: SANCHO, VAN DIJK, DEMBELE, AKE, MERTENS, VERTONGHEN, LONG - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 12 February 2020

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 12.02.2020: SANCHO, VAN DIJK, DEMBELE, AKE, MERTENS, VERTONGHEN, LONG


Mchezaji anayepiganiwa na man United kwa kipindi kirefu

Manchester United iko tayari kuipiku Chelsea katika kinyang'anyiro cha kutoa dau la £120m kumsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19. (Mirror)

Liverpool inajiandaa kumpatia beki wa Uholanzi Virgil van Dijk, 28, mkataba mpya wenye thamani ya zaidi ya £150,000 kwa wiki. (Football Insider)

Manchester United inaweza kufufua hamu yake ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 Moussa Dembele mwisho wa msimu huu (L'Equipe, via Manchester Evening News)

Beki wa Liverpool anayepiganiwa na Barcelona

Tottenham inaandaa dau la £40m ili kujaribu kumsajili beki wa kati wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, (Express)

Mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32, ana uwezekano mkubwa kuondoka katika klabu hiyo kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu huku Chelsea, Manchester United na Arsenal zote zikipigania saini yake. (Mail)

Chelsea Itamchunguza mchezaji wa Morocco Hakim Ziyech kwa kipindi cha msimu kilichosalia ili kuweza kumnunua mchezaji huyo wa Ajax katika dirisha la mwezi Januari mwaka ujao.



Manchester City, Manchester United, Liverpool na Atletico Madrid zote beki wa Verona na Albania Marash Kumbulla, 20. (Gazzetta dello Sport, via Sport Witness)

Mshambuliaji wa Southampton na jamhuri ya Ireland Shane Long, 33,natarajiwa kutia saini kandarasi mpya katika klabu hiyo huku mkataba wake ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu . (Southern Daily Echo)

Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho alitazama mechi ya sare ya 0-0 ya Bayern Munich dhidi ya RB Leipzig siku ya Jumapili , huku beki wa Leipzig na Ufransa Dayot Upamecano, 21, akiwa mmoja ya wachezaji aliokua akitaka kumsajili. (Mirror)

Aston Villa inajiandaa kuipatia Crystal Palace dau la £15m ili kumnunua mshambuliaji wa Norway Alexander Sorloth, 24, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo na klabu ya Uturuki ya Trabzonspor. (Turkish Football)

-BBC

No comments:

Post a Comment