Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Mhandisi Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya Serikali kwenye mdahalo kati ya NMB na Wakandarasi kutoka Kanda ya Ziwa. |
BENKI ya NMB mwaka jana imetoa
zaidi ya dhamana 500 kwa wakandarasi wazawa
ili kuwawezesha kugharimia miradi mbalimbali
ya ujenzi nchini. Mkakati huo ulifikiwa
kufuatia kilio cha muda mrefu cha
wakandarasi kushindwa kushiriki katika ujenzi wa
miradi mbalimbali kutokana na ukata wa
fedha na ushindani toka kwa makampuni ya
nje.
Akiongea
wakati wa kongamano lililohudhuriwa na
zaidi ya wanadarasi 300 kutoka Kanda ya
Ziwa mwishoni mwa wiki, Afisa Mkuu wa
Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa
NMB Filibert Mponzi alisema zoezi hilo litakua endelevu.
Alisema
mbali na kusaidia kuwanyanyua wakandarasi
wadogo kimtaji, pia Benki hiyo imeitikia
wito wa Rais John Magufuli alioutoa juu
ya taasisi mbalimbali za kibenki kuwakopesha
wakandarasi kwa masharti nafuu. “Kama benki
ya biashara na kama mbia wa serikali
tumeshiriki kikamilifu kuwasaidia wakandarasi kimtaji
na pia kuitikia wito wa Rais Magufuli
kuhakikisha kada hiyo inashiriki kikamilifu
katika ujenzi wa uchumi,” alisema Mponzi.
Mkakati wa
kutoa dhamana kwa wakandarasi umesaidia
sana kuwawezesha kupata kazi za uhakika za
ujenzi na kwa mujibu wa Mponzi benki
inatoa dhamana ya asilimia 50 ya thamani
ya mradi husika. Mbali na kutoa dhamana
ya mikopo NMB pia itaanza kutoa
huduma ya bima kwa waka ndarasi hao
kuwawezesha kushiriki kwa ufanisi zaidi
kwenye miradi mbalimbali kwa riba nafuu.
Hata
hivyo, alisema wakati benki ikibuni njia
mbalimbali za kuwasaidia wakandarasi wadogo na
wazawa kuna umuhimu mkubwa kwao kuwa
waaminifu katika urejeshaji wa mi kopo na
kuheshimu masharti ya dhamana ili kuepuka
kulipa riba kubwa kama adhabu baada
ya mikataba kukiukwa.
Katika
kongamano hilo lililohudhuriwa pia na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eliud Mwakalinga
wakandarasi walijadili chan gamoto mbalimbali na
kushauri mikakati mbalimbali ya kupambana nazo.
Akizungumza
nao, Katibu Mkuu Mwakalinga mbali na
kuishukuru NMB kwa ubunifu na huduma za
mikopo na dhamana kwa wakandarasi wazawa
alisema kazi za ujenzi zinahitaji uaminifu
mkubwa na kuzi ngatia ubora. Alisema tafiti
mbalimbali zinaonesha wakandarasi wazawa hasa
wadogo wamekuwa wakishindwa kupewa kazi kubwa
kwa zababu kadhaa zikiwamo wengi kushindwa
kuajiri wahandisi waliobobea na wenye
weledi usiotiliwa shaka.
“Tumefanya
utafiti na kugundu a kuna shida kubwa
kwa wakandarasi wengi wadogo kushindwa kukaa
na wahandisi waliobobea kwa kukwepa kuwalipa
mishahara wanayostahili na kuishia kuajiri
wahandisi wanafunzi na hata mafundi mchundo
tu,” alisema.
Mhandisi
Mwakalinga alidokeza mbinu kadhaa za kuwawezesha
wakandarasi wadogo ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha wanashindana katika kujenga miradi
mikubwa inayoshikiriwa na makampuni mengi
ya nje.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha
Wakandarasi Mkoani Mwanza Mhandisi Oscar Munishi
aliwataka wakandarasi wazawa kujitathmini juu ya
uadilifu wao kazini na kwamba kuna
mapungufu kadhaa yanayohitaji kufanyiwa kazi
miongoni mwao. Aliyashukuru mabenki yaliyojitokeza
kuwadhamini kwa mikopo ya riba nafuu na
akaishukuru NMB kwa kukutana nao na
kujadili nao namna ya kuboresha utendaji kazi
na kushindana kikamilifu sokoni.
#NMBKaribuYako
No comments:
Post a Comment