NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 5 February 2020

NCHI ZA SADC ZATAKIWA KUTATHMINI UCHUMI WAKE BILA KUTEGEMEA MASHIRIKA YA KIMATAIFA PEKEE

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipeana mkono na Kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Sikhumbuzo Dlamini, baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao, Jijini Dodoma.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) na Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (kushoto), wakiwa katika Mkutano katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.


Kiongozi wa Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bw. Sikhumbuzo Dlamini akifafanua jambo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayupo pichani), ambapo aliipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayofanya katika kukuza uchumi.

Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wakifuatilia mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Ujumbe kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), ukiongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (hayupo pichani) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), uliongozwa na Bw. Sikhumbuzo Dlamini (wa nne kulia), pamoja na viongozi wa Wizara hiyo na wajumbe kutoka SADC, Jijini Dodoma.


Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma

WAZIR
I wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa nchi za Afrika hasa zilizopo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zinatakiwa kujitazama na kushauriana kuhusu mwenendo wao wa uchumi badala ya kuyaachia Mashirika ya Kimataifa pekee.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dodoma wakati wa Mkutano kati yake na Ujumbe wa SADC unaoongozwa na Bw. Sikumbuzo Dlamini, ambao umetembelea nchini kwa ajili ya Mpango wa kujitathmini kiuchumi kwa mwaka wa Fedha 2019/20.

Dkt. Mpango alisema kuwa nchi za Afrika zimezoea kuona Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) au kuja kuangalia namna gani Uchumi unavyoendelea ili hali   Afrika hasa nchi za SADC zina fursa pia ya kutembeleana na kushaurina namna bora ya kuendeleza uchumi na kuwahudumia wananchi ikizingatiwa kuwa nchi hizo zinafahamiana vizuri.

“Madhumuni ya ujumbe wa SADC kutembelea nchini ni kuangalia hali ya ukuaji wa uchumi, ubadilishanaji wa fedha za kigeni, mauzo ya bidhaa ndani na nje ya nchi na kushauri mahali ambapo Tanzania haijafanya vizuri au kutumia fursa ipasavyo’’, alieleza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa nchi za SADC zilikubaliana kuchagua ujumbe ambao utakuja nchini kufuatilia namna uchumi Mkuu unavyoendelea, hivyo ametumia fursa hiyo kueleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya Umeme wa Maporomoko ya Mto Rufiji, ujenzi wa Reli kwa kiwango cha Kimataifa (SGR) na miundombinu mingine ya barabara.

Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa SADC, Bw. Sikumbuzo Dlamini, ambaye pia ni Meneja wa Sera za Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Eswatini, ameipongez Tanzania kwa maendeleo makubwa iliyofikia baada ya kujionea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Reli, miradi ya maji ambayo itasaidia ukuaji wa uchumi Uchumi Mkubwa na kuiwezesha kufikia Malengo ya Maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment