Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu (katikati), akishiriki ujenzi wa hosteli ya wasichana katika Sekondari ya Puma. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Alixandrina Katabi na Mjumbe wa kamati ya Siasa, Diana Chilolo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ameishukuru Serikali kwa kutoa sh.milioni 140 kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli na madarasa katika shule za sekondari jimboni humo.
Shule zilizopata msaada huo ni Shule ya Sekondari ya Puma ambao wamepata sh.milioni 75 kwa ajili ya ujenzi wa hosteli za wasichana na Shule ya Sekondari ya Msungua iliyopo Kata ya Sepuka iliyopata sh.milioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Kingu alitoa shukurani hizo wakati akishiriki ujenzi wa hosteli hiyo katika uzinduzi wa sherehe za kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika mapema wiki hii.
Alisema kukamilika kwa ujenzi wa hosteli hizo kutaongeza ufaulu kwa wanafunzi hao kwani watapata muda mzuri wa kujisomea wakiwa shuleni tofauti na sasa ambapo wanatumia muda mwingi kwa kutembea kutoka majumbani kwao kwenda shuleni.
"Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais wetu Dkt.John Magufuli kwa msaada huu ambao unakwenda na tamko lake la kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.
No comments:
Post a Comment