Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi aliyesimama akizindua
Jukwaa la Haki Jinai Mkoa wa Singida. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Mashitaka(DPP) Nchini, Biswalo Mganga na kulia in Katibu Tawala Mkoa wa
Singida Dkt. Angerina Lutambi.
Picha ya pamoja baina ya Mkrugenzi wa Mashitaka, (DPP) Biswalo Mganga
mwenye suti, Mkuu wa Mkoa wa Singida (mwwnye kilemba) anayefuata
Dkt. Angelina Lutambi Katibu Tawala Mkoa wa Singida na wajumbe wa Jukwaa
la Haki Jinai Mkoa wa Singida Mara baada ya kuzinduliwa kwa Jukwaa hilo
la Mkoa.
Baadhi ya watumishi wa Umma Singida walioshiriki kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Haki Jinai Mkoa wa Singida (Picha Zote na John Mapepele, Singida.
Na John Mapepele, Singida
Dkt. Nchimbi amesema kuzinduliwa kwa Jukwaa hili kutakuwa
nguzo kuu ya kuzima uhalifu katika Mkoa wa Singida, huku akiwataka wajumbe
kutumia jukwaa hili kufanya utatifi na
kutafakari kwa kina ni namna
gani bora ya kudhibiti uhalifu
badala ya kusubili utokee na kupeleka kesi mahakamani, jambo
ambalo amesema madhara yake
yamekuwa makubwa.
“Namshukuru Mungu. Leo, kwangu ni siku ya kihistoria na ya
kipekee ambayo nilitamani kuona inatimia tangu siku nyingi. Kila wakati nimekuwa
nikiwasisitiza kuwa ni muhimu na ni
lazima vyombo vyote vya Serikali katika mkoa wetu kufanya kazi ya
kupambana na uhalifu kwa pamoja
badala ya kila mmoja kujiona ni bora zaidi katika nafasi yake jambo halina tija na halitusaidii kama taifa, lakini hatimaye
leo hili linatimia” alisisitiza
Aidha amewataka Wajumbe kufanya kazi kwa umoja
na uzalendo ili jukwaa hilo liwe
mfano bora na mikoa mingine waje kujifunza.
“Kama kwenye mambo mengine tumeweza kushika nafasi za kwanza kitaifa kwa nini tusiwe wa kwanza katika
kufanya kazi nzuri kwenye kutekeleza majukumu ya jukwaa la Haki Jinai
kwenye Mkoa wetu na wengine waje kujifunza kwetu, inawezekana endapo kila mtu
atatekeleza wajibu wake” alisisitiza
Dkt. Nchimbi
Dkt. Nchimbi
amesema hata vitabu
vitakatifu vimeandika mwisho ya
uhalifu ni mbaya na kwamba msharaha wa dhambi ni mauti na kuelekeza kuwa kila Ofisi
na Idara ya Serikali katika Mkoa
wa Singida kuwa na mfumo wa Jukwaa la Haki Jinai ambao utasaidia
kujenga mfumo wa kutafakari na kudhibiti
uhalifu badala ya kusubiri utokee.
Amesema ili kuwa na ufanisi na tija wa kutokomeza uhalifu kwenye Mkoa wake
ameyataka majukwaa ya Haki Jinai ya kila
Wilaya kuanza mara moja kufanya kazi na kupeleka mapendezo yake
katika Jukwaa la Mkoa kwa kuwa Jukwaa la Mkoa linategemea utendaji wa
majukwaa ya Wilaya.
Akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida
kabla ya uzinduzi huo , Mganga amesema
kwa mujibu wa Sheria ya Mashitaka na 27 ya mwaka 2008 ibara ya 59(B) (II) na kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Mkurugenzi wa
Mashitaka ndiye mwenye jukumu la kuratibu upepelezi wa kesi zote za jinai nchini japokuwa
anaweza kukasimu madaraka hayo kwa
vyombo vingine vya Serikali.
Amesema Ofisi yake
imedhamilia kutokomeza uhalifu wa
kijinai kwa kutekeleza mkakati wa kuunda
kwa majukwaa ya Haki Jinai kila Mkoa hapa nchini ambalo
ni takwa la kisheria ili
kuwa muarobani wa kuthibiti matukio na kesi za kijinai badala ya kusubiri
makosa yafanyike na kutoa hukumu jambo ambalo amesema halina tija
kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Mganga amesema kwa kuzingatia
ukubwa wa tatizo na ongezeko wa uhalifu wa kijinai Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Rais, John Pombe Joseph Magufuli iliamua kufanya marekebisho makubwa ya kupambana na tatizo hili ambapo
iliunda Ofisi ya Taifa ya Mashitaka
kwa kutangaza kwenye gazeti la Serikali namba 49, tarehe 13/2/2018 tofauti na awali ambapo Kurugenzi ya
Mashitaka (DPP) ilikuwa chini ya
Ofisi ya Mwanasherioa Mkuu wa Serikali.
Amewataka wajumbe wote
wanaounda jukwaa hilo
kufanya kazi kwa weredi na kushirikiana
ili kuhakikisha mazingira ya
shughuli za kijinai yanakwenda vizuri ambapo amesema majukwaa ya Mkoa yanatakiwa kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kwenye Jukwaa la Haki Jinai la Taifa kwa
ajili ya utekelezaji na ufuatiliaji.
Amesema kuliungana na Sheria ya Mashitaka, Jukwaa la Haki
Jinai la Mkoa linatakiwa kukaa vikao visivyopungua viwili kwa
mwaka ambapo amesisitiza wajumbe kuhudhuria wao wenyewe badala ya
kuja wawakilishi kwa kuwa sheria
inawataka wajumbe halisi na sio wawakilishi na kuongeza kuwa kama kunakuwa na ulazima au umuhimu, vikao hivyo ninaweza
kuketi zaidi ya mara mbili kwa mwaka kadri ya mahitaji.
Mkurugenzi, Mganga ameelekeza
Jukwaa la Haki Jinai Mkoa wa Singida kuanza kazi mara mmoja ili kutatua
changamoto mbalimbali zinazokabili
uhalifu katika mkoa ambapo amelitaka
kuketi mara mbili kabla ya Oktoba
mwaka
Mwenyekiti wa Jukwaa la Mkoa wa Singida, Rose Chilongozi ambaye ni Mwendesha Mashitaka Mkoa wa Singida
alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa
kuzindua Jukwaa hilo na kumhakikishia
kuwa yeye na wajumbe wake watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili
kudhibiti uhalifu katika mkoa
huo.
Katibu wa Jukwaa la
Haki Jinai Mkoa wa Singida ambaye
ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa huo,
Kamishina Msaidizi wa Polisi, Stela Mutabihirwa amewataja wajumbe wa
Jukwaa hilo kuwa ni pamoja na Mwendesha Mashitaka wa Mkoa ambaye ni
Mwenyekiti, Mkuu wa upelelezi wa Mkoa ambaye ni Katibu, Mkuu wa Usalama wa
Taifa wa Mkoa,
Wengine ni Afisa Ustawi wa Mkoa, Mwenyekiti wa Bodi ya Parole wa Mkoa, Afisa Mkemia Mkuu wa Mkoa, Afisa-Bwana Huruma wa Mkoa, Mwanasheria
kutoka Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa na Afisa
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa na mdau mwingine yoyote ambaye wataona
anafaa kumwalika kushughulikia jambo husika.
Kamishina Msaidizi wa
Polisi Mutabihirwa ambaye ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Singida
amesema kwa upande wa Polisi anaishukuru
Serikali kwa kuharakisha kuzindua jukwaa
hilo kwenye Mkoa wa Singida kwa kuwa litasaidia
kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu.
“Napenda kumshukuru Mheshimiwa, Rais Magufuli kwa kuunda
chombo hiki kupitia Ofisi ya Mashitaka
kwani kwa sisi Jeshi la Polisi tutashikisha dawati letu la Polisi Jamii ambapo sasa naamini tutatoa elimu mashuleni na kupunguza mimba za utotoni pia uhalifu wa
mauaji, ukatili wa kijinsia na migogoro
ya ardhi na mashamba ya wananchi katika
Mkoa wetu itapata ufumbuzi wa kudumu”
ameongeza Afande Mutabihirwa
Akifungua rasmi kikao cha uzinduzi wa Jukwaa hilo Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina
Lutambi amesema kila mwananchi anawajibu
wa uzuia uhalifu ili Mkoa wa Singida uwe sehemu salama.
Aidha aliwaasa wajumbe
kufanya kazi kwa kuzingatia
sheria ili kuwa ukuta imara wakuzuia
aina yoyote ya uhalifu ambao unaweza kupenya
na kuingia makao makuu ya nchi.
No comments:
Post a Comment