Mahakama ya juu ya Pietermaritzburg
nchini Afrika Kusini imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi
hiyo, Jacob Zuma baada ya kushindwa kufika mahakamani kukabiliana na
mashtaka kuhusu rushwa dhidi yake.
Hati hiyo itafanya kazi ikiwa
atashindwa kuhudhuria kesi yake itakayoanza mwezi Mei. Bwana Zuma
anakabiliwa na makosa 16 ya kughushi, rushwa , ulaghai na utakatishaji
fedha ukihusisha biashara ya silaha ya thamani ya mabilioni ya dola
iliyofanywa tangu miaka ya 1990.
-BBC
No comments:
Post a Comment