Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha Mashauriano baina ya Serikali na sekta binafsi kilichofanyika mkoani Simiyu jana. |
Na Munir Shemweta, WANMM SIMIYU
NAIBU WAZIRI wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini
kuanza kupanga maeneo ya uwekezaji katika sehemu ambazo miji inakuwa kwa kasi.
Dkt Mabula alisema hayo
jana katika mkutano wa Mashauriano baina ya Serikali na sekta binafsi kuhusiana
na changamoto za uwekezaji katika mkoa wa Simiyu.
Alisema, kuna maeneo
mengi nchini ambayo miji inaendelea kwa kasi hivyo halmashauri kupitia
Wakurugenzi wake zinapaswa kuhakikisha zinatenga maeneo ya uwekezaji kwa lengo
la kumuwezesha Mwekezaji atakapopatikana asipate tabu.
‘’Ni vizuri katika
kipindi hiki ambacho baadhi ya miji inakuwa kwa kasi halmashauri zikatenga
maeneo ya uwekezaji na kuyahaulisha kwa lengo la kuwarahisishia wawekezaji
watakapokuja kuwekeza katika halmashauri husika’’ alisema Mabula
Aidha, Naibu Waziri
Mabula amezitaka pia halmashauri kuhakikisha zinapanga miji maeneo yaliyopo
pembezoni kwa kuanishwa matumizi yake kama vile kilimo, ufugaji na maeneo ya
kuchezea kwa kutumia watendaji wa ngazi za chini badala ya kusubiri wataalamu
wa mipango miji.
Alisema, upangaji miji
mapema kwa kutumia watendaji wa ngazi za chini utasaidia wataalamu wa mipango
mijini watakapokuja baadaye kutopata shida katika kupanga maeneo hayo hasa katika
ile miji inayokuwa kwa kasi kwa kuwa miji hiyo itakauwa imepangwa na kuainisha
matumizi mbalimbali.
‘’Hawa watendaji wa
chini wakipewa elimu wataweza kuipanga miji yao kama ilivyokuwa wakati wa
vijiji vya ujamaa maana sasa hivi mtu anaweza kujenga kiwanda katikati ya
makazi ya watu’’ alisema Mabula.
Katika mkutano huo
Manaibu Mawaziri kutoka sekta mbalimbali walitolea ufafanuazi baadhi ya
changamoto zilizowasilishwa kwao kwa lengo la kurahisisha ufanyaji biashara
itakaokuwa na tija.
Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Ashatu Kijaji alitoa ufafanuazi wa riba kubwa kwa taasisi na fredha
na kubainisha kuwa serikali ya awamu ya tano imesikia kilio hicho na imekuwa
ikisisitiza taasisi hizo kupunguza riba kufikia asilimia kumi na moja.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima alisema lengo la serikali si
kufungia biashara bali ni kutafiuta njia itakayowawezesha wawekezaji kufanya
biashara katika mazingira mazuri na kubainisha kuwa mtendaji wa ofisi yake
atakayekwamisha jitihada hizo basi taarifa itolewe ili hatua zichukuliwe.
Naye Naibu Waziri wa
Ujenzi Elias Kwandikwa alisema, wizara yake inafanya jitihada kubwa kuunganisha
mikoa katika masuala ya miundombinu sambamba na kushughulikia maeneo korofi ili
wawekezaji wafanye kazi zao kwa urahisi.
Mnaibu Mawaziri wengine
waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Viwanda
na Bishara Stela Manyanya, Maliasili na Utalii Constatntine Kanyasu na kiongozi
wa mkutano huo Angela Kairuki Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji.
No comments:
Post a Comment