JPM: NENDENI MKATANGULIZE UZALENDO KWANZA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday 3 February 2020

JPM: NENDENI MKATANGULIZE UZALENDO KWANZA

Rais wa Jumhuri  ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, akisisitiza jambo kwa viongozi wa Wizara mbalimbali na Taasisi za Serikali mara baada ya kuwaapisha Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020.

Makatibu Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu  wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Nishati na Wizara ya Ardhi, Makamishina wa Jeshi la Magereza na Zima moto na Viongozi wengina wa Serikali wakiwa katika hafla ya kuapishwa kwao  Ikulu Jijini Dar es Salaam, baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli.


Rais wa Jumhuri  ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kulia waliokaa) na Jaji Mkuu Ibrahimu Jumaa ( kushoto waliokaa)  wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, TAMISEMI, Nishati, Katiba na Sheria, Mambo ya Ndani, Viwanda, Habari pamoja na viongozi walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam, Februari 03, 2020. 


Na Eric Msuya - MAELEZO

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi walioapishwa kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za uongozi pamoja na kuwa na   hofu ya Mungu bila kusahau kutanguliza Uzalendo katika kuhakikisha Tanzania inafikia malengo iliyojiwekea.
Rais Magufuli Ameyasema hayo leo tarehe 3 Februari 2020 katika hafla ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni. 
“niwapongeze sana kwa majukumu yenu mapya ambayo nina amini mtakwenda kuyafanyia kazi kwa Uzalendo wa Kweli na bila Kusahau Kumtanguliza Mungu  na kufanya kazi kwa kufuata sheria katika utendaji kazi wenu huko mnapoenda” amesema Rais Magufuli
Sambamba na hilo Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kumpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya HabariUtamaduniSanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kwa utendaji kazi wake katika kuisemea Serikali. 
“Dkt. Abbasi umefanya kazi nzuri sana kwa kuisemea vizuri Serikali, nakupongeza sana kwa kuteuliwa  kuwa Katibu Mkuu hivyo utaendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali hii mpaka atakapopatikana mtu mwingine “ amesema Rais Magufuli
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amemshukuru Rais Magufuli kwa kujaza safu na kuteua Viongozi   katika mahakama hivyo kwenda kurahisisha upatikanaji wa huduma. 
“Nashukuru Rais magufuli  kwa kuendelea kujaza safu za mahakama, umetupatia viongozi ambao wana weledi wa kazi hii ya mahakama, hivyo nina amini kabisa tunaenda kufanya kazi a kuwatumikia watanzania” amesema Jaji Mkuu
Miongoni mwa walioapishwa leo na Rais Magufuli  ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wizara ya Nishati, Bi Zena Ahmed Said, katibu Mkuu Wizara ya Viwanda  Riziki Shemdoe, Katibu Mkuu wizara ya mambo ya ndani ya Nchi Christopher Kadilo, Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Bi Marry Gaspar  Makondo.
Wengine walioapishwa leo na Rais Magufuli  ni Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Steven Mhoja Mashauri,  Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Emmanuel Mpawe Kukube, Naibu katibu Mkuu  wizara ya nishati Leonard Robert Masanya.
Kwa upande kwa Mahakama Viongozi walioapishwa ni Msajili Mkuu wa mahakama ya Tanzania Wilbert Chuma, Msajili wa Mahakama ya Rufani Kelvin David, pamoja na Kamishna wa Magereza  Brigedia Jenerali Suleiman Mzee na Kamishna wa Jeshi la zima moto na uokoaji John Wiliam.

No comments:

Post a Comment