Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae akizungumza na waandishi wa habari |
Kundi la Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan |
Mnyama Ngiri akiwa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan akila majani |
Mamba akiwa pembezoni mwa Mto Wami unaopita kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan |
Watalii
kutoka maeneo mbalimbali dunia wakiwa kwenye magari ya wazi wakitalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan
HIFADHI ya Taifa ya Saadani imesifu juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt John Magufuli kuendeleza sekta ya Utalii hapa nchini kutokana na uwekezaji wa usafiri wa anga ambao umewawezesha watalii kufika moja kwa moja nchini.
Hayo
yalisemwa na Afisa Utalii wa Hifadhi ya Saadan Athumani Mbae wakati
akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo ambapo pia
alisema serikali ya awamu ya tano imefanya kazi kubwa ya uboreshaji
miundombinu.
Ambapo
alisema hilo limesaidia ongezeko la watalii kutokana na wageni wengi
kuthamini sana muda ambapo sasa wageni wanaau wezo wa kwenda mahali
popote bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote.
Hata
hivyo Afisa Utalii huyo alisema pia suala jambo jingine ambalo
limefanywa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt Magufuli na kuwa
na tija kubwa kwao kuitendaji ni mabadiliko ya mfumo wa kutoka kwenye
kufanya kazi kiraia kwenda Jeshi Usu.
Alisema
kwani majangili hao wamekuwa ni nia mbaya ya kuihujumu serikali kwenye
hifadhi hivyo uwepo wa mfumo huo umesaidia kupunguza changamoto za namna
hiyo na kuwawezesha wanyama kuzidi kuongeza kwenye hifadhi.
Akizungumzia
mfumo wa ukusanyaji wa mapato kwa eletroniki kwa njia ya mtandao
umekuwa ni muhimu sana kwao kwani mepunguza viatarishi kutokana na watu
kubeba fedha zao mkononi na wanapofika getini wanalipa.
“Lakini
kwa sasa hauihitaji kutembea na fedha kwenye mkoba bali unalipa kwa
mfumo wa mtandao ambao umerahisisha wageni wanapoingia kutokana na
viatarishi vya kubeba pesa taslimu mkononi”Alisema
No comments:
Post a Comment