Na Ahmed Mahmoud,Arusha
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema gereza Kuu La Arusha limeshindwa kufikia malengo ya kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya wafungwa katika mkoa huo.
Masauni amesema hayo jana Jijini Arusha wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika gereza hilo kwa ajili ya kufuatilia hali ya uzalishaji katika sekta ya kilimo haswa zao la maharage na mahindi.
Alisema serikali inalazimika kutumia kiasi cha shilingi milioni 800 kwa ajili ya kununua chakula cha kulisha wafungwa katika gereza hilo jambo ambalo siyo sahihi.
"Mnamiliki hekari 900 halafu mnalima hekari677 pekee na chakula hakitoshi kulisha wafungwa huu ni uzembe haikubaliki"
Alisema ni hasara kwa serikali kuendelea kununua chakula wakati kuna nguvu kazi kubwa ya wafungwa ambao wamengweza kuzalisha mazao ya chakula cha kutosha kulisha gareza hilo na magereza ya mikoa mingine.
Kwa mujibu wa Masauni magereza hiyo imeshindwa kitekeleza agizo la rais John Magufuli la kuzitaka magareza zote nchini kulima kilimo chenye tija ili waweze kujitegemea kwa chakula badala ya serikali kununua chakula cha wafungwa.
Kutokana na kilimo hicho kusua sua Masauni alilazimika kuwasiliana na Kamshina wa magereza nchini na kumtaka kuleta kiasi cha shilingi milioni 326 kwa ajili ya kuwezesha kilimo cha umwagiliaji.
Alisema ni aibu kwa magereza hiyo kukosa kiasi hicho vha fedha licha ya kuwa na shamba kubwa pamoja na miradi mingine ikiwemo ya ufugaji na kutaka kiasi hicho cha fedha kitumike kwa malengo yaliyokusudiwa na si vonhinevyo.
Kwa upande wake mkuu wa gereza kuu la ArushaAndrew Mtamamiro alikiri ni kweli wameshindwa kufikia malengo ya uzalishaji wa chakula kwa ajili ya wafungwa na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote ya Naibu waziri Masauni.
No comments:
Post a Comment