Muonekano wa madarasa yaliyojengwa na kukaribia kutumika kwa wanafunzi wa shule za msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. |
Walimu wakuu washule mbalimbali za msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni wakikagua madarasa yanayojengwa wakati wa ziara na Afisa Elimu Msingi
wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni. |
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imetumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi
na ukaratabati wa vyumba 107 vya madarasa pamoja na matundu ya choo 157 kwa
wanafunzi wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri hiyo.
Hayo yamebainisha
na Afisa elimu msingi wa Halmashauri hiyo Kiduma Mageni wakati wa ziara ya
kukagua miradi mbalimbali ya shule iliyokuwa na lengo la kuona maendeleo ya
miradi hiyo ambayo inatekelezwa kwa kutumia Force Account.
Akizungumza mara
baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, Ndugu Mageni alisema kuwa katika fedha hizo
zilizotumika kujenga na kukarabati vyumba hivyo vya madarasa pamoja na matundu
ya choo, shilingi milioni 771, 520,000 zinatokana na makusanyo ya ndani,
shilingi milioni 455,140,000 ni pesa kutoka serikali kuu kupitia mpango wa EP4R.
Aidha Mageni
ameongeza kuwa katika fedha hizo pia kiasi cha shilingi milioni 210, 004, 726
ni pesa kutoka mpango wa madarasa 100 ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Daniel
Chongolo, na kiasi cha shilingi milioni 4, 140,000 nipesa zinazotokana na nguvu
za wananchi.
Sambamba na hivyo,
ndugu Mageni amebainisha madarasa yaliyojengwa ni 58, yaliyokarabatiwa ni 42 na kwamba kwa vyumba vilivyokarabatiwa
vimeanza kutumika na wanafunzi huku vile vinavyojengwa vikiwa vimekamilika kwa asilimia
95.
Mageni
amesema Halmashauri ya Kinondoni kupitia Mkurugenzi Aron Kagurumjuli pamoja na
Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
kuwa inajenga na kukarabati madarasa hayo ili wanafunzi waweze kusoma katika
mazingira mazuri.
Ameongeza kuwa
Serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli inatoa
elimu bure na kwamba viongozi hao Mkurugenzi Kagurumjuli na Mkuuwa Wilaya Chongolo
wanaitekeleza kikamilifu sera hiyo.
“
Niwapongeze sana kwa kazi nzuri wanayoifanya, tumejionea wenyewe wanafunzi
wanakaa kwenye majengo mazuri,ya kisasa ,mengine bado yapo kwenye hatua ya
mwisho kukamilika na muda sio mrefu
yatakabidhiwa ili watoto wetu wa anze
kuyatumia.
“Nampongeza
sana Mhe. Chongolo, Kagurumjuli na timu
yake yote wanafanya kazi kubwa,
inaonekana, Rais wetu Dk. Magufuli ametoa elimu bure na sisi tunaitekeleza, nasio
kwamba tunaishia hapa, bado tutaendelea kutekeleza zaidi na zaidi ili watoto
wetu wasome kwenye majengo safi” alisema Mageni.
Mageni
amesema ameridhishwa na ujenzi, ukarabati wa majengo hayo na hivyo kuwataka
walimu hao kuwa wasimamizi wazuri wa miundombinu hiyo.
Kwa upande wa
mwalimu hao waliokuwa katika ziara hiyo wamempongeza Mkurugenzi Kagurumli kwa kuwezesha
ujenzi wa madarasa hayo na kwamba wanafunzi watasoma kwa nafasi.
Mmoja wa
walimu hao ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge, Janeth Mlenge
alisema kuwa elimu bure inayotolewa na Rais Dk.Magufuli imetoa hamasa kwa
wazazi na hivyo kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma.
Mwalimu Mkuu
wa shule ya Msingi Nyakasanga amesema kuwa kupitia mradi huo katika shule yake
amejengewa vyumba nane vya madarasa ofisi ya mwalimu mkuu pamoja na matundu 13 ya choo na hivyo
kumpongeza Mkurugenzi Kagurumjuli,Mhe. Chongolo kwa kuwapatia majengo hayo.
Hata hivyo
walimu hao wameonyesha kufurahishwa na huduma hiyo ya kujengewa madarasa katika
shule zao, sambamba na kukarabatiwa na kusema serikali kupitia Halmashauri ya
Kinondoni inatekeleza vema sera ya Elimu bila malipo.
No comments:
Post a Comment