SERIKALI KUTOKUWAVUMILIA WANAOTUMIA VIBAYA FANI YAUNUNUZI NA UGAVI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Friday, 6 December 2019

SERIKALI KUTOKUWAVUMILIA WANAOTUMIA VIBAYA FANI YAUNUNUZI NA UGAVI

Kamishana wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Frederick Mwakibinga, akitoa taarifa fupi ya maadhimio yaliyopitishwa kwa ajili ya utekelezaji  kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, ambae ni mgeni  rasmi kabla ya kufunga Kongamano la Kumi la Waatalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC – Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, (katikati), akiimba wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Kongamano la Kumi la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) lililofanyika Dodoma. Wengine kutoka kushoto Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi (STAMICO), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Godfrey Mbanyi, Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Frederick Mwakibinga, na Mwakilishi kutoka Kenya Bw. Peter Momanyi.

Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Kumi la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPSTB), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, (hayupo pichani), wakati akifunga Kongamano la Kumi la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), katika ukumbi wa DCC, Jijini Dodoma.

Na Peter Haule na Josephine Majura – Dodoma

SERIKALI imesema kuwa haitamvumilia mwanataaluma ya Ununuzi na Ugavi atakayesababisha upotevu  wa rasilimali za nchi kwa kutozingatia kanuni na sheria. Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Shaaban, alipokuwa akifunga Kongamano la 10 la Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) zaidi ya 600 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Bi. Amina Shaaban alisema kuwa fani ya Ununuzi na Ugavi ni adhimu na inalojukumu kubwa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kati uliojikita katika Viwanda ambapo fani hiyo ni muhimu upatikanaji wa bidhaa na huduma.

“Yeyote atakayepata nafasi ya kiutendaji, anapaswa kuzingatia miiko na maadili ya fani ya ununuzi na ugavi kama anavyoongozwa na sheria katika kusukuma juhudi za maendeleo. Atakaye kwamisha juhudi za Serikali katika kukuza uchumi wa viwanda na kutoa huduma bora kwa wananchi asifumbiwe macho wala kuhurumiwa”, alisema Bi. Amina Shaaban.

Alisema kuwa anafurahishwa na hatua ya Bodi ya PSPTB ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ili waweze kushiriki kikamilifu katika hatua mbalimbali za kukuza uchumi wa viwanda.

Amewataka wataalamu wote waliohudhuria katika Kongamano hilo, kutekeleza maazimio yote waliyokubaliana nayo  na  kufanya tathimini ya kiutendaji. Kwa upande wake Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Fredrick Mwakimbinga alisema kuwa washiriki wamejadili mada mbalimbali na kuelekezana kuhusu umuhimu wa fani hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda na pia wamekumbushwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi, uzalendo na kufuata sheria.

No comments:

Post a Comment