SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday, 17 December 2019

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NA MADARAJA-NAIBU WAZIRI KWANDIKWA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (kulia) akipata maelezo alipokuwa akikagua athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (hayuko pichani) akikagua athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Muonekano wa ujenzi wa madaraja ukiendelea wilayani Kilindi mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akisikiliza kero za wanakijiji wa Kwediboma wilayani Kilindi, Mkoa wa Tanga katika ziara yake.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) akizungumza na wananchi alipokuwa katika ziara yake kukagua athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa akiwa katika ziara hiyo na viongozi wengine alipokuwa akikagua athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja iliyoathiriwa na mvua ili kuhakikisha huduma za usafiri na uchukuzi nchini kote haziathiriki na mvua hizo.

Naibu Waziri, Kwandikwa amesema hayo katika Mji wa Kibirashi wilayani Kilindi mkoani Tanga wakati akikagua athari za mvua kwenye miundombinu ya barabara na madaraja eneo hilo.

Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi uharibifu wa barabara na madaraja unapotokea ili ushughulikiwe na kupunguza ajali zinazoweza kujitokeza.

"Tumejipanga kuhakikisha barabara zote nchini zinapitika wakati wote," alisisitiza Naibu Waziri, Kwandikwa akizungumza katika ziara hiyo ya ukaguzi.

No comments:

Post a Comment