RAIS DK MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA MPEMBA-ISONGOLE KM 50.3 TUNDUMA MKOANI SONGWE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday 5 October 2019

RAIS DK MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA TUNDUMA PAMOJA NA UJENZI WA BARABARA YA MPEMBA-ISONGOLE KM 50.3 TUNDUMA MKOANI SONGWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo ili kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma katika eneo la Mpemba Tunduma mkoani Songwe.

Mfano wa hospitali hiyo ya Halmashauri ya Mji wa Tunduma utakavyokuwa mara baada ya kukamilika.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Viongozi wengine kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa barabara ya Mpemba-Isongole km 50.3 itakayojengwa kwa kiwango cha lami.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi  wa Mbozi wakati akielekea Mpemba mkoani Songwe.


No comments:

Post a Comment