NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMTAKA MKANDARASI BARABARA YA MWENGE-MOROCCO KUONGEZA KASI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 29 October 2019

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMTAKA MKANDARASI BARABARA YA MWENGE-MOROCCO KUONGEZA KASI


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akisalimiana na wafanyakazi wanaojenga barabara ya Mwenge-Morocco Km  4.5  jijini Dar es Salaaam.



Muonekano wa Barabara ya Mwenge-Morocco Km 4.5 ambayo upanuzi wake unaendelea jijini Dar es Salaaam.



Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam Eng. Julias Ngusa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa alipokagua ujenzi wa Barabara Mwenge-Morocco Km  4.5  jijini Dar es Salaam.



Kazi ya Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco Km 4.5 ikiendelea jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akisisitiza jambo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam, Eng. Julias Ngusa.


Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam Eng. Julias Ngusa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa alipokagua ujenzi wa Barabara Mwenge-Morocco Km  4.5  jijini Dar es Salaam.



Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias John Kwandikwa akizungumza na wanahabari baada ya kukagua barabara ya Mwenge-Morocco Km 4.3.


NAIBU
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa amemtaka Mkandarasi NIPPO-DAI NIPPON JV anayejenga Barabara ya Mwenge Morocco Km 4.5 kuongeza kasi ya ujenzi huo ili ukamilike mapema mwakani.

Naibu Waziri Mhe. Kwandikwa ametoa maelekezo hayo leo jijini Dar es Salaam alipokagua ujenzi wa barabara hiyo na kusisitiza ujenzi huo uendane na uwekaji mifereji ya kupitisha maji ili kuepuka mafuriko katika eneo hilo.

"...Zingatieni ubora katika ujenzi wa barabara hii na hakikisheni mifereji ya kupitishia maji inakuwa na uwezo wa kupitisha maji ya mvua ili kuepuka mafuriko," amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Dar es salaam Eng. Julias Ngusa amesema TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam wamejipanga kuhakikisha ujenzi wa barabara hiyo unakamilika kama ilivyopangwa na kwa ubora unaotakiwa.

Amewataka watumiaji wa barabara hiyo kwa sasa kuwa wavumilivu na kutii maelekezo ya wajenzi wa barabara hiyo ili kuepuka ajali na kuwawezesha kufanyakazi zao vizuri.

Naibu Waziri Mhe. Kwandikwa yupo jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku tatu kukagua miundombinu maeneo mbalimbali.

No comments:

Post a Comment