MAKAMISHNA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA 'HAWATEKELEZI' MAJUKUMU YAO - WZIRI HASUNGA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 26 October 2019

MAKAMISHNA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA 'HAWATEKELEZI' MAJUKUMU YAO - WZIRI HASUNGA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal)

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiongoza kikao kazi na Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.


 Mwenyekiti wa Tume y maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kanani  akizungumza wakati wa kikao kazi cha Tume hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma, tarehe 25 Octoba 2019.


Na Mathias Canal, Dodoma

WAZIRI wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa Makamishana wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.

Amesema kuwa Mali zinaibiwa za wananchi, watu wanauziana viwanda huku Ubadhilifu ukiwa umekithiri kuliko kawaida lakini bado kuna tume ya Maendeleo ya Ushirika.

Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Makamishna wa Tume hiyo katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo tarehe 25 Octoba 2019.

Waziri Hasunga amesema kuwa jumla ya Bilioni 124 zimeibiwa kwenye vyama vya ushirika lakini hakuna hatua zilizochukuliwa, "Mnataka mpaka kuwe na posho ndipo kamati ikutane kuona ulazima wa kusimamia fedha na Mali za ushirika" Alihoji Mhe Hasunga

Aliongeza kuwa wizi wa mali na fedha hizo za ushirika ni ishara ya makamishna kutofanya majukumu yao ipasavyo hivyo jambo hilo linapelekea Wanachama kuendelea kuteseka.

"Nasikitika sana Watu walioaminiwa na kupewa dhamana wameshindwa kutekeleza majukumu yao, kwenye zao la ufuta pekee zimeibiwa Bilioni 2.5 lakini wahusika wanadunda mtaani kadhalika mazao kama ya korosho na Pamba ambapo hakuna Ushirika badala yake kuna madalali tu" Alisema

Mhe Hasunga ameongeza kuwa hakuna sababu ya kuwa na Tume ya Ushirika isiyotekeleza majukumu yake ipasavyo huku akiongeza kuwa serikali inataka kujenga ushirika lakini kuna watu kazi yao ni kubomoa, na kuweka urasimu katika utendaji.

Waziri Hasunga amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya ushirika Dkt Titus Kanani kuchukua hatua za haraka kwa watendaji wote wa Tume hiyo ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mhe Hasunga amesema kuwa endapo ushirika utasimamiwa vizuri wananchi watakuwa na maendeleo maradufu yatakayopelekea Taifa kuendelea mbele kiuchumi.

Kadhalika ametoa nafasi ya ziada kwa Tume hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha matokeo makubwa ya uwajibikaji vinginevyo ametishia kuivunja tume hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt Titus Kamani amempongeza Waziri wa Kilimo kwa kukubali kushiriki katika kikao hicho huku Kamishna wa Tume hiyo Mudhihir M. Mudhihir akizungumza kwa niaba ya Makamishna wengine amehakikisha kuwa Tume hiyo itatekleza majukumu yake kwa weledi mkubwa.

No comments:

Post a Comment