WIZARA YA FEDHA WAASWA KUZINGZTIA SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 9 July 2019

WIZARA YA FEDHA WAASWA KUZINGZTIA SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA

Katibu Mkuu wa Wizara  ya Fedha na Mipango  Bw. Doto James (kushoto) akifungua kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma, Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila akijibu hoja katika kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara  ya Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dodoma.
 
Na Josephine Majura, Dodoma

WATUMISHI wa Wizara ya Fedha ya Mipango wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yaoWito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James wakati wa kikao cha watumishi wa Wizara hiyo.

Bw. James alisema kuwa watumishi wote wanawajibu wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi  wote wanaohitaji huduma katika Wizara yetu” Alisema Bw. James.

Aidha Bw. James aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyopishwa na Bunge hivi karibuni na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Bajeti hiyo.

Kwa upande wa Watumishi wa Wizara hiyo waliupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili pamoja na kuzitolea ufafanuzi.

Waliahidi kutatekeleza maelekezo yote aliyotolewa kwa uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment