KITENGO CHA MALALAMIKO MAMBO YA NDANI CHATUPIA JICHO WILAYANI KILOMBERO - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 17 July 2019

KITENGO CHA MALALAMIKO MAMBO YA NDANI CHATUPIA JICHO WILAYANI KILOMBERO

Ofisa wa Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko Kivaula Msigwa wa Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi akitoa maelekezo kwa baadhi ya wawakilishi wa wananchi 54 kutoka Kijiji cha Ihenga, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro baada ya kusikilizwa, kuhudumiwa malalamiko yao ya kunyang’anywa mashamba na mwekezaji Kilombero Farm na kubambikiwa kesi ya kuvamia mashamba na kutishia amani kwa mwekezaji.

Baadhi ya wawakilishi wa wananchi 54 kutoka Kijiji cha Ihenga, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro wakipanda gari chini ya usimaziwa Maofisa kutoka Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko kwenda kwa Kamishna wa Ardhi, baada ya kutoka katika Kitengo hicho kilichopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo walifikisha malalamiko ya kunyang’anywa mashamba na mwekezaji Kilombero Farm, kubambikiwa kesi ya kuvamia mashamba na kutishia amani kwa mwekezaji.

Baadhi ya wawakilishi wa wananchi 54 kutoka Kijiji cha Ihenga, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro wakiwashukuru Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kitengo cha Kushughulikia Malalamiko baada ya kusikiliza  malalamiko yao ya kunyang’anywa mashamba na mwekezaji Kilombero Farm, kubambikiwa kesi ya kuvamia mashamba na kutishia amani kwa mwekezaji.

No comments:

Post a Comment