WMO INAMCHANGO MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA TANZANIA - NDITIYE - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Tuesday 11 June 2019

WMO INAMCHANGO MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA TANZANIA - NDITIYE

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye.

Na Christopher Philemon, Monica Mutoni, Geneva

NAIBU Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye ameeleza namna ambavyo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linavyochangia katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania.  Mhe. Nditiye alizungumza hayo wakati akihutubia mkutano wa 18 wa WMO, unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

‘WMO ina mchango mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini kama vile miongozo maalum iliyowekwa kwa ajili ya uandaaji na utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya ziwa Viktoria ambapo TMA inatoa miongozo ya tahadhari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utekelezaji wa Mfumo wa Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services-GFCS) ambao ndani yake Tanzania kupitia TMA inanufaika masuala mbalimbali kama vile mafunzo ya muda mrefu na mfupi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa n.k’ alisema Mhe. Nditiye.

Aidha, katika hotuba yake, Mhe. Nditiye aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuelezea namna serikali inavyoweka jitihada kubwa kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za kisasa kwa kufanikisha ununuzi wa rada tatu za hali ya hewa pamoja na kuifanya TMA iweze kukidhi zaidi matakwa ya watumiaji kwa kuibadilisha TMA kutoka kuwa Wakala na kuwa Mamlaka kamili.

Wakati akimalizia hotuba yake, Mhe. Nditiye alitumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii nchini na kumnadi mgombea wa nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi kutokana na uwezo na uzoefu alionao WMO akiwa mjumbe wa kamati kuu wa shirika hilo kwa miaka saba.

No comments:

Post a Comment