WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUA MAONESHO YA WAJENZI YA MWAKA 2019 DODOMA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 15 June 2019

WAZIRI KIGWANGALLA AFUNGUA MAONESHO YA WAJENZI YA MWAKA 2019 DODOMA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua Maonesho ya Wajenzi mwaka 2019 jijini Dodoma leo, maonesho hayo yamehusisha makampuni yanayojishughulisha na ujenzi zaidi ya 50. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi  na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma  Bw. Godwin Kunambi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa  na makampuni ya ujenzi wakati wa Maonesho ya Wajenzi kwa mwaka 2019 jijini Dodoma.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma maelezo ya huduma alipotembelea banda la maonesho la Kampuni ya Mwanza Plastic Limited (MPL) wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa za plastiki yakiwemo mabomba ya maji wakati wa maonesho ya Wajenzi kwa mwaka 2019 jijini Dodoma leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia vifaa vya umeme vinavyozalishwa na makampuni ya Tanzania wakati wa maonesho ya Wajenzi ya mwaka 2019 jijini Dodoma leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kuhusu bidhaa za rangi kutoka kampuni ya Jotun mara baada ya kufungua Maonesho ya Wajenzi kwa mwaka 2019 jijini Dodoma leo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Maonesho ya Wajenzi kwa mwaka 2019 jijini Dodoma leo. PICHA/ Wizara ya Maliasili na Utalii.

No comments:

Post a Comment