MBUNGE RITTA KABATI ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA YA UDAKTARI PHD - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday 19 June 2019

MBUNGE RITTA KABATI ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA YA UDAKTARI PHD


 Rais wa  Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) Dk. Donald (kushoto), akimpongeza Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati  baada ya Chuo cha Africa Graduate University cha Lusaka nchini Zambia kumtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD)  katika mahafali ya 37 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki nchini Zambia.

 Makamu Mkuu wa Chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sierra Leone, Profesa Timothy Kazembe (kushoto), Katibu Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel wakiwa na Mbunge Kibati baada ya kutunukiwa Tuzo hiyo.

Rais wa  Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) Dk. Donald  (katikati), Makamu Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University, Profesa Timothy Kazembe (kushoto) awakiwa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Iringa,  Ritta Kabati  baada ya chuo hicho  kumtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD)  katika mahafali ya 37 ya chuo hicho yaliyofanyika mwishoni mwa wiki nchini Zambia.
Katibu Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), Stellah Joel, akimpongeza Mbunge Kibati baada ya kutunukiwa Tuzo hiyo.

Na Dotto Mwaibale

CHUO cha Africa Graduate University cha Lusaka nchini Zambia kimemtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Iringa Ritta Kabati pamoja na Watanzania wengine wanne.

Waliotunukiwa tuzo hizo za heshima ni wale waliotoa mchango mkubwa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea za kijamii na zikaleta manufaa kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa njia ya simu wakati wa mahafali ya 37 ya chuo hicho, Makamu Mkuu wa Chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sierra Leone, Profesa Timothy Kazembe, alisema kila mwaka kimekuwa kikitoa Tuzo za heshima na Shahada za Uzamili kwa Watanzania waliotoa mchango wa kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali.

"Tunao watunuku tuzo hizi za heshima ni watu waliokuwa na umri wa miaka 60 ambao wanafanya kazi za kijamii katika nyumba za ibada kwa zaidi ya miaka 15 na kuendelea na wale ambao umri wao ni miaka 40 hadi zaidi na wenye shahada," alisema Profesa Kazembe.

Mbunge Ritta Kabati ametunukiwa Tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa wa kufanya shughuli mbalimbali za kujitolea za kijamii pamoja na kusaidia watu wenye ulemavu.

Wengine Waliotunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari ni Bishop Dk. Daniel Kwiyeya wa Zanzibar, Mhandisi Dk. Elina Kayanga wa Tarula Dodoma, Dk. William Henry wa Tanga pamoja na Dk. Ester Sollo ambaye ni mwanaharakati wa kusaidia vikundi mbalimbali vya wanawake.

Baadhi ya watanzania wengine waliowahi kutunukiwa Tuzo na chuo hicho ni Askofu Dk. Godfrey Mallasy, Ofisa wa Jeshi la Polisi Dk. Ezekiel Kyogo, Mtakwimu Dk. Margaret Mutaleba, Mwanahabari Dk. Tumaini Msowoya, Mwanaharakati wa Haki za Watoto ambaye ni Rais wa Tanzania Music Foundation Dk. Donald Kisanga, Dk. Mlute Nyasa, Dk. John Pallangyo, Dk. Wilson Nyiti na Dk. Godwin Maimu. 

No comments:

Post a Comment