Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Ryata akizungumza na wananchi wa Kata ya Ruaha na Kitwiru juu ya maendeleo ya Manispaa hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya wakiwasikiliza madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakielezea sera zao na mikakati juu ya maendeleo ya Manispaa ya Iringa.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
NAIBU Meya wa Manispaa ya Iringa
kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Ryata amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha
wanaboresha miundombinu ya uchumi ili kukuza ukchumi kwa wananchi na kuleta
maendeleo kwa taifa.
Akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Ruaha, Ryata alisema kuwa watahakikisha
barabara zote za Manispaa ya Iringa
zinapitika kirahisi ili kuhakikisha kuwa zinapitika na zinakuwa rafiki kwa
wafanyabiashara kufanya biashara zao.
“Wananchi tusipokuwa na
miundombinu bora ya barabra hatuwezi kufanya biashara na kupata maendeleo
yanayaotakiwa hivyo ni lazima tuwasimamie viongozi wetu wa serikali kuhakikisha
barabara zote zinapitika bila kuwa na vikwazo kwa wafanyabiasha na wananchi kwa
ujumla,” alisema Ryata
Ryata aliongeza kuwa madiwani
wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasimamia
vilivyo ujenzi wa gorofa katika maeneo ya standi ilipokuwa tembo bara na kuboresha
kwa kuujenga upya ukumbi wa Community center ulipo katika kata ya Kitanzini
Miomboni na kujenga hoteli ya kitalii katika kata ya Gangilonga.
“Tukiboresha miundombinu hiyo yote na kujenga
majengo ya kibiashara yatatusaidia kukuza uchumi wa wananchi wa manispaa ya
Iringa na nje ya manispaa ya Iringa hivyo mipango hii inasimamiwa vilivyo na
madiwani wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa,” alisema Ryata
Ryata aliwataka wananchi wa manispaa ya Iringa
kuhakikisha wanaendelea kuwachagua viongozi wa chama cha mapinduzi ili waweze
kusaidia kuleta maendeleo kwa haraka na ubora unaotakiwa tofauti na viongozi
wengi wa upinzani hawana hoja za
kiuchumi.
Naye Diwani wa Kata ya Ruaha Tandesi Sanga alisema
kuwa wamefanikiwa kuboresha miundombimu ya sekata ya afya, elimu pamoja na
miundombinu ya uchumi kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanafanya
kazi za maendeleo bila ya kuwa na usumbufu wowote ule.
“Nyie mashaidi toka nimekuwa diwani wa CCM tumefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya majengo ya
shule zetu za sekondari na msingi na zahanati zetu tumeziboesha mno hivyo
lazima tufanye kazi kama Rais wetu anavyotutaka,” alisema Sanga.
No comments:
Post a Comment