KIUMA COMMUNITY HOSPITAL. |
* Amejenga
shule, hospitali na vyuo akizalisha ajira
Na Adam Mwambapa, Tunduru
TAKRIBAN mwendo wa saa 12 umbali wa kilometa 965 unanifikisha
KIUMA. Kitongoji kilichopo kijiji cha Milonde, Kata ya Milonde, Tarafa ya
Matemanga, Wilaya ya Tunduru na mkoa wa Ruvuma.
Dhumuni kubwa ni kukutana na Dk. Matomorwa Matomorwa.
Ambaye sifa zake zimeenea sehemu mbalimbali nchini na zaidi sanamikoa ya Kusini
kama, Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Akiwa ni miongoni mwa watu wanaoguswa sana na hali duni
ya kiuchumi, za wakazi wa ukanda huo. Ingawaje najisikia uchovuwa safari uliopitiliza, unaochangiwa
na kukaa kwenye gari muda mrefu huku nikiwa nimebadilisha mikao isiyokuwa na
idadi kamili.
Ila nafarijiwa na jambo moja, nalosi lingine zaidi ya
lengo la ujio wangukijijini hapo kutimia. Hili ndilo kuu. Ninapoingia kwenye geti la mlango wa Kanisa la Upendo wa
Kristo Masihi (KIUMA), ambalo ndilo lililobeba jina la kitongoji. Siachi
kushangaa!
Kwa nini? Mbele yangu kulia naliona jengo lililo na
maandishi ‘KIUMACOMMUNITY HOSPITAL.’ Naelezwa
kuwa, hiyo ni hospitali yenye uwezo wa kualaza wagonjwa wapatao 100 kwa wakati
mmoja! Na kushoto kwangu ni jengo la Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA).
Wakati ndani ya ua ‘fence’, kumesheheni majengo ya nyumba za watumishi
ambao jumla ya idadi yao naelezwa ni 464, huku idadi kubwa ya wafanyakazi
wakiwa ni Waislamu.
Waama kwa hakika nastaajabishwa sana, kujua ukubwa wa
taasisi niliyoiendea na jitihada zilivyo za kukwamua tatizo la ajira nchini. Lakini pia kuna majengo yashule, viwanja vya michezo
mbalimbali, kumbi za mikutano na chakula, hosteli na vyuo mithili ya kijiji kinachojitegemea.
Ndimo mnamomeremeta kwa mwangaza
wa taa chekwaa. Napata ‘mgagasiko wa moyo,’ na maswaliyasiyo idadi.
Je, ni nishati ipi ya umeme
iliyofanikiwa kuangaza eneo lote hili, ambalo naambiwa lina umbali wa kilomita
tano mpaka sita za mraba? Au je, mradi wa umeme vijijini (REA) wameshafika eneo
hili? Najiuliza hivi,kwa kuwa ni umeme unaowaka humu ndani na si eneo lote la
kijiji.
Wenyeji hawaachi kunijulisha kuwa,ni
nishati itokanayo na jenereta kubwa sana iliyowekwa na Dk. Matomorwa kwa juhudi
zake, ndiyo iliyowezesha kupang’arisha hapo.
Napumzika kwa lengo la kutimiza ahadi ya kukutana na Dk. Matomorwa siku ya kesho yake, ili aweze kunijulisha kuyaelewa haya na mengineyo.
Ninapata bahati ya kukutana na Dk. Matomorwa, anayeanza kueleza matatizo ya mikoa ya Kusini yalivyo na jinsi wanavyojisikia kutengwa kimaendeleo tafauti na mikoa mingine nchini.
“Kimsingi sisi watu waKusini,
tumelelewa kwenye ‘culture’ moja ya muda mrefu bila kuingiliwa na watu kutoka
nje. Historia inayoanzia tangu tunapata uhuru, ambapo Tanzania ilikuwa na
Majimbo nane moja likiwa ni Kusini,”anaeleza Dk. Matomorwa.
Anasema kutengwa kwao kulianza
hata katika michezo. Wakati huo Majimbo yote nane yalikutana Dar es Salaam,
ilikuwa ni rahisi sana kwao Jimbo la Kusini kupangwa na timu nzuri ili ifungwe
tu; basi!
“Wazee wa Yanga na Simba wakati
huo ‘Sunlight’ walikuwa wakipangiwa na timu kali kidogo inayojua mpira, kwa
hiyo walikuwa wakifungwa goli nane au 11; na asubuhi saa 12 wanapanda gari
kurejea Lindi,”anaendelea kueleza.
“Hiki kikawa kipimo kizuri cha
unyonge wetu.Kwani hatukuwa na cha ziada kwetu. Tumepata uhuru sawa kwa hulka,
lakini Jimbo hili likagawanyika. Na wakati huohuo Makao Makuu ya Jimbo
yakapelekwa Mtwara…..Mtwara na Lindi ni pua na mdomo, na kuna maendeleo kidogo.
Tatizo ni sisi hapa katikati tunaoripoti mkoa wa Ruvuma, ni nani atapaangalia
hapa?”anahoji.
Kwa mujibu wa maelezo yake
anasema hata ukienda kwenye idara yoyote ya Serikali, iwe wizarani au wilayani
kwa sasa, uulize ni lini na ni kiongozi yupi aliyewahi kuja hapa kwetu KIUMA au
Matemanga? Hutapata jibu.
Hii ni kwa sababu, hakuna
kiongozi yeyote anayewiwa au kuumizwa na hali ya unyonge wetu tulionao. Na
pengine sababu kubwa ni umbali ulipo.
Kadhia nyingine kubwa anayoiona
Dk. Matomorwa, iliyokuwa ikiwatenganisha na kuwatofautisha na wengine kutoka mikoa
mingine, ni idadi ya wanafunzi waliokuwa wakisoma Shule ya Sekondari Mkwawa
iliyokuwa Iringa enzi hizo.
Anasema kwa miaka ile 1964, jumla
ya idadi ya wanafunzi wote waliokuwa wanasoma shule ya Mkwawa ilikuwa ni400.
Hii ilikuwa nikutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Lakini kutoka Kusini walikuwa
wanafunzi saba tu; huku aliyetoka Tunduru akiwa ni mmoja tu ambaye ni yeye.
“Wanafunzi wa Tanga, Arusha na
Moshi walikuwa wakiletwa na mabasi manne, wakati wanafunzi wa Tabora na Mwanza
mabasi mawili na Mbeya basi moja; mabasi yaliyoingia hadi shuleni kuwashusha
wanafunzi ndani,”anaeleza na kuendelea:
“Lakini sisi tutokao Kusini, ilitosha
tu kuja nausafiri wa Relwe ambao nao haukutufikisha hadi shuleni.Wakawa wakitushusha
stesheni kulingana na uchache wetu,”anaeleza kwa uchungu.
Dk. Matomorwa ambaye pia ni
Askofu na muasisi wa KIUMA anasema, kitendo hicho ndicho kichochangia fikra
hasi, hasira wakati fulani na kuhoji kwa
nini sisi Kusini hali zetu ni duni kiasi hiki?Hali hii mpaka lini?
Anasema kuwa, wenzaowa Lindi, Songea,
Mtwara, Masasi na Ndanda walikuwa na maendeleo kidogo yenye tija tofauti na
huku kwao anakotambulisha kama Kusini Kati. Kwa sababu, maeneo hayo mengine wao
walikubali na kuwaruhusumapema Wamissionari waingie kwao.
Ndiyo maana huko Ndanda kuna
shule za tangu awali, Peramiho kuna huduma za hospitali tangu hapo.
“Liuli, Litembo, Lituhi na
nyinginezo, ni matokeo ya wenzetu kuwapokea Wamissionari awali na maendeleo
wanayojivunia. Sisi hapa,mtawala wetu mkuu chifu Mataka alihakikishaWamissionari
hawaingii na zaidi sana alikuwa anawafukuza,”anaeleza Dk. Matomorwa.
Anazidi kutoa maelezo ya kina kwa
kusema, wakati huo ndiyo maana Serikali ya Kizungu ilishindwa kufanya lolote
lenye maendeleo kwetu….kwa kuwa, kwa huduma za kijamii Serikali ya Kizungu iliwaachia
Wamissionari.
Kanisa la Upendo wa Kristo Masihi (KIUMA). |
No comments:
Post a Comment