WANAWAKE MSD WATOA MSAADA WODI YA KANGAROO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 9 March 2019

WANAWAKE MSD WATOA MSAADA WODI YA KANGAROO HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

 Wanawake wa Bohari ya Dawa (MSD), wakishusha vitu mbalimbali walivyotoa kwa wanawake wenzao na watoto waliozaliwa kabla ya wakati waliopo wodi ya Kangaroo Hospitali ya Taifa ya Muhili jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

 Aneth Moshi wa MSD, akimkabidhi Maria Mzee Ali msaada huo.

 Meneja Jengo la Wazazi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Stellah Rushagara, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kupokea msaada huo.

 Mwenyekiti wa Wanawake MSD, Rehema Mosha, akizungumza. Kushoto ni Selwa Hamid.

 Misaada ikitolewa.

 Mama akipokea msaada.

 Dada Selwa Hamid wa MSD, akikabidhi msaada.

Msaada ukitolewa

Na Dotto Mwaibale

JAMII imetakiwa kujenga tabia ya kuwasaidia wenzao wenye changamoto mbalimbali za maisha ikiwemo magonjwa.

Mwito huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa Wafanyakazi Wanawake wa Bohari ya Dawa (MSD) Rehema Mosha wakati wanawake hao walipokuwa wakitoa msaada ya vitu mbalimbali kwa akina mama ambao wamelazwa na watoto wao waliozaliwa kabla ya kutimiza miezi tisa wodi ya Kangaroo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)

"Ni vizuri jamii ikabadilika na kuwa na moyo wa kusaidia makundi yenye changamoto kama hawa wakina mama wenzetu ambao wapo katika hospitali hii kwa muda mrefu wakiwa na watoto wao" alisema Mosha.

Alisema wao kila mwaka katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wamejijengea utaratibu wa kuchangishana na kununua vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia kundi fulani watakaloona linahitaji msaada ambapo kwa mwaka huu wakaona waende katika wodi hiyo ya Kangaroo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt. Faraja Chiwanga alitoa shukurani kwa wanawake wa MSD kwa msaada huo na kueleza kuwa ni wa muhimu ukizingatia kuwa wakina mama  wengine wanatoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam hivyo hawana jamaa wa kuwasaidia.

Alisema watoto hao waliozaliwa kabla ya wakati wanakuwa kupitia joto la kifua cha mama zao ambapo wakati wote wanatakiwa kukumbatiwa na wanakuwa bila ya wasiwasi wowote.

"Hawa watoto kama mnavyowaona wanatakuwa kama kawaida kupitia joto la mama zao na kesho mtasikia kuwa ndio viongozi wa baadae" alisema Dkt. Chiwanga.

Mama ambaye alijifungua mapacha kabla ya wakati, Mariam Salum mkazi wa Kitunda, alitoa shukurani kwa MSD kwa niaba ya wenzake kwa msaada waliowapatia na kusema upendo huo wauendeleze na kwa watu wengine.

No comments:

Post a Comment