WARSHA YA WANAHABARI ILIYOANDALIWA NA TMA KUJADILI MSIMU WA MVUA WA MWEZI MACHI HADI MEI 2019 - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 13 February 2019

WARSHA YA WANAHABARI ILIYOANDALIWA NA TMA KUJADILI MSIMU WA MVUA WA MWEZI MACHI HADI MEI 2019

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a akifungua warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).

Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri - TMA, Bw. Samwel Mbuya akiwasilisha mada katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 

Mtaalamu (Utabiri) wa Hali ya Hewa, Elias Lipiki  akiwasilisha mada kwa wanahabari katika warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Law School of Tanzania Mawasiliano jijini Dar es Salaam. 

Mwanahabari Faustin Shija kutoka Nipashe, akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA.

Jerome Mshanga wa Clouds Media akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA kwenye warsha hiyo.

Mwanahabari na Bloga, John Bukuku akitoa uzoefu wake juu ya upokeaji na usambazaji wa taarifa za TMA.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a akifafanua jambo kwenye warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).
Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo imetoa warsha kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).

Akifungua warsha hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang'a alisema warsha hiyo muhimu inalenga kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua na kufanya tathmini ili kuboresha zaidi taarifa za utabiri.

Alisema TMA itaendelea kutoa elimu kwa wanahabari kwani ni kiungo na wadau muhimu katika utoaji na usambazaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa nchini.

"..Naomba mtambue kuwa wanahabari ni kiungo muhimu cha usambazaji wa taarifa zetu na tunathamini sana michango yenu ndio maana tunawashirikisha...," alisema Chang'a akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi.

Aidha aliwaomba wanahabari kuzingatia warsha wanazopata kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini na kuwa mabalozi wazuri wa taasisi hiyo katika kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa.


No comments:

Post a Comment