Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala akizungumza na waandishi wa habari kufafanua wateja walivyojishindia zawadi anuai kwenye Masta Bata ya NMB. |
Meneja wa NMB Tawi la Mlimani City, akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika kwenye tawi lake. |
SHINDANO la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata', leo limeendelea kuchezeshwa huku wateja sita wakijishindia simu janja za kisasa 'Samsung S9+' zenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/- kila moja.
Katika droo hiyo ya nne pia wateja 20 wengine wa benki hiyo wamejishindia fedha taslimu shilingi 100,000/- ambazo zitaingizwa kwenye akaunti zao moja kwa moja ndani ya saa 24 tangu kuchezeshwa kwa droo hiyo. Droo hiyo ya nne iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imefikisha wateja 80 hadi sasa ambao wameshindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuchezeshwa droo ya leo, Meneja Mwandamizi kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Manfredy Kayala alisema mbali na droo hiyo kupata washindi 20 wa shilingi 100,000/- kila mmoja, wateja 6 wengine wamejishindia simu aina ya Samsung S9+' kila mmoja yenye thamani ya shilingi milioni 2,300,000/-.
Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia zawadi hizo.
Hata hivyo, aliwaomba wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika na shindano hilo.
No comments:
Post a Comment