SHINDANO la Benki ya NMB kuhimiza matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' linalojulikana kama 'MastaBata', limefanyika tena ikiwa ni droo ya tatu ambapo wateja wa benki hiyo wameendelea kujishindia fedha taslimu kwenye akaunti zao. Droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam imewapata washindi wengine 20 waliojishindia kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja.
Akizungumza katika droo hiyo leo, Mtaalamu kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya NMB, Florence Mchau alisema wateja wengine 20 wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja katika droo hiyo ya tatu kuchezeshwa, baada ya kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass'.
Alisema wateja hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa droo iliyojumuisha wateja wote wa NMB waliolipa au kufanya manunuzi kwa kutumia mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' na wao kujishindia kitita hicho.
Aidha droo ya tatu iliyofanyika leo inakamilisha jumla ya idadi ya wateja 60 ambao hadi sasa wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja, huku ikiendeshwa kwa wazi ambapo wateja wakipigiwa simu na kujulishwa kabla ya kuingiziwa fedha walizojishindia.
Hata hivyo, aliwataka wateja wa NMB kuendelea kutumia huduma hiyo, kwani kampeni hiyo inayotarajia kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 100 wateja wa NMB inaendelea na takribani wateja 200 watanufaika.
Licha ya fedha zawadi nyingine ambazo washindi watajipatia ni pamoja na simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu na NMB.
Droo hiyo ikiendelea kuchezeshwa kushoto huku wakishuhudia |
No comments:
Post a Comment