Dk. Ali Mohamed Shein. |
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema
hatua ya Serikali kutangaza elimu bila malipo Septemba 23, 1964, ililenga
kuwakombowa kielimu watoto wa wanyonge wa Taifa hili.
Alisema
kabla ya Mapinduzi matukufu ya 1964, watoto wa kimaskini walikosa kabisa fursa
ya kupata elimu, kutokana na kukosa uwezo wa kuigharamia.
Dk.
Shein amesema hayo leo huko Bwefuu
katika hafla ya Ufunguzi wa skuli ya msingi na Sekondari ya Bwefum, ikiwa ni
miongoni mwa shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Alisema
kabla ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa na skuli chache ambapo watu wenye uwezo
pekee ndio waliopata fursa ya kupeleka watoto wao kupata elimu.
Alisema
katika ukanda wa maeneo ya Kiembesamaki hadi Bwefum, kulikuwa na skuli chache
zilizojengwa, ikiwemo skuli ya msingi
Kombeni iliyojengwa mwaka 1935, Kiembe samaki (1943) na Bwefum mwaka 1956.
Alieleza
skuli ya mwanzo ambayo ilitumika zaidi kwa watoto wa Kiafrika ilikuwa ni skuli
Dole, iliyojengwa mwaka 1935, sambamba na skuli ya Uzini, Wilaya Kati Unguja.
Alieleza
kuwa Mapinduzi ya 1964, yameifanya
Zanzibar kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu, na kubainisha
kuwa kabla ya Mapinduzi hayo kulikuwa na
skuli zisizozidi 60, wakati ambapo hivi sasa zimefikia zaidi ya 400.
Aidha
alisema Zanzibar hivi sasa ina vyuo vikuu vitatu, wakati ambapo miaka 22
iliyopita hakukuwa na chuo kikuu hata kimoja.
Dk.
Shein alirudia kauli yake kwa kuwataka wazazi na walezi kutokuchangia mahitaji
ya kielimu kwa watoto wao, kwa vile serikali tayari imefuta michango yote
katika skuli za msingi na Sekondari.
Alifafanua
kwa kusema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya uchumi kuimarika kutokana na
ukusanyaji bora wa kodi pamoja na misaada mbali mbali ya washirika wa maendeleo
na wawekezaji wazalendo.
Akitowa
mfano, alisema wakati anaingia madarakani mwaka 2010 Serikali ilikuwa
ikikusanya kodi ya shilingi Bilioni 13.5 kwa mwezi, wakati hivi
sasa inakusanya wastani wa shilingi Bilioni 65 kwa kipindi kama hicho.
"Hii
sio kazi ya mchezo ni kazi nzuri inayofanywa na taasisi zetu za kukusanya
kodi,....... nami sitaki mchezo katika suala la ukusanyaji wa kodi, sina msalie
mtume katika suala hilo", alisema.
Aliwapongeza
baadhi ya wafanya biashara wenye nia njema na serikali kwa kulipa kodi kwa
hiari, huku akiwaasa wale wenye tabia ya kukwepa kulipa kodi.
Alisema
kiwango hicho kikubwa cha ukusanyaji kodi kinathibitisha utekelezaji bora wa
Ilani ya CCM, akibainisha matarajio makubwa ya kufikiwa kwa malengo kabla ya
wakati uliopangwa.
Aidha,
aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kusimamia na kuhoji mwenendo wa mapato ya Serikali, pale
panapotokea mashaka.
Alieleza
kuwa ukusanyaji bora wa mapato ndio unaoiwezesha serikali kutekeleza malengo
yake ya maendeleo, kupitia sekta mbali mbali, kama vile elimu, afya, viwanda na
nyenginezo.
Alisema
Zanzibar ni miongoni mwa nchi chache katika Bara la Afrika zinazotowa elimu
bure, akiitaja Tanzania Bara kufanikiwa katika suala hilo, huku Kenya ikiweka
azma ya kufanya hivyo.
"Lakini
sisi tumeanza tangu 1964 na hadi leo tunaendelea, tumezishinda nchi nyingi
zenye uwezo mkubwa ", alisema.
Aidha,
alisema hatua hiyo imefungua fursa ya kuongezeka kwa madarasa ya skuli za
msingi ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi, hatua aliyoinasibisha na kuongezeka
kwa idadi ya watu nchini, ambapo kabla ya Mapinduzi Zanzibar ilikuwa na watu
wapatao 300,000, wakati hivi sasa imefikia Milioni moja na nusu.
Katika
hatua nyengine, Dk. Shein alisema Serikali imepunguza kiwango cha kupokea
misaada kutoka kwa washirika wa maendeleo, kutoka asilimia 30.2 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 7.2 hivi sasa,
akibainisha kiwango hicho kuzidi kupungua mwaka huu pamoja na mikopo.
Aidha,
alimpongeza Rais mstaafu awamu ya tano Dk. Salmin Amour Juma kwa kupanga maeneo
ya Fumba na Micheweni kuwa ya Uwekezaji, kwa lengo la kuyabadili maeneo hayo na
hivyo watu wake kupata heshima kubwa.
Alisema
Serikali inakusudia kuyaendeleza maeneo hayo ili kuimarisha jamii hiyo na
maendeleo ya miji yake.
Aliongeza
kwa kusema kuimarika kwa maeneo hayo kumewafanya wageni mbali mbali wanaozuru
Zanzibar kushajiika kuyatembelea ili kujionea maendeleo makubwa yaliofikiwa.
Alieleza
kuwa amefursahishwa sana na wananchi wa maeneo hayo kuridhia uwekezaji huo na
hivyo kunufaika na maendeleo yanayojiri kila kukicha.
Aliwapongeza
watu wa Bwefum na kuwataka kuongeza nguvu na mapenzi kwa serikali yao.
Aidha,
aliipongeza Kampuni ya Union Property Developers Ltd kwa kujitolea na kujenga
skuli hiyo, hivyo akawataka wana Bwefum kuthamini hatua hiyo kuwa ni neeema
kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Aliwasihi
wasizibeze na kuzikufuru neema kama hizo, pamoja na kuwataka wawekezaji hao
kuendeleza misaada yao kwa maendeleo ya Zanzibar.
Akigusia
kauli ya baadhi ya watu 'wasiojielewa ' ya kumhusisha na madai ya kuwadanganya
wananchi kisiwani Pemba kwa kudai kuwa hakuna maendeleeo yoyote yaliofikiwa,
Dk. Shein alisema kauli hiyo kamwe haiwezi kuwavunja moyo wananchi, kwa vile
maendeleo yanayozungumzwa yamekuwa aykionekana na kila mwenye macho.
Aidha,
aliweka bayana kuwa suala la utiaji saini mkataba wa mafuta na gesi asili kuwa ulifanyika
hadharani na kufuatiliwa na vyombo kadhaa vya habari, hivyo kupinga madai ya
watu hao kuwa ulifanyika kwa siri.
"Kama
ile inaitwa siri, dhihiri inaitwaje?", alihoji.
Akigusia
kauli Za watu hao na Muungano, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa
1964, ulikuwa ni wa hiari na kubainisha kuwa miongoni mwa wale wanaoutia dosari
Muungano huo, walikuwepo Serikalini wakati ulipokuwa ukiundwa.
Aidha,
Dk. Shein alisema Sherehe za Mpinduzi zitafanyika kisiwani Pemba na kuwaonya
wale wote wenye lengo la kuvuruga sherehe hizo.
"Tumeamuwa
kwa makusudi sherehe kuzifanya kisiiwani Pemba, tulijuwa wataumwa, sasa kama
kuna yeote mwenye ubavu tutaona", alisema.
Aliwakakikishia
wananchi kuwa Serikali imejiimarisha katika suala la ulinzi katika mji wa
Zanzibar pamoja na kununua vifaa vipya kwa ajili ya shughuli za usalama
baharinin nchini kote.
Waziri
wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma alimpongeza Rais wa
kutowa fursa kwa Wawekezaji wazalendo kusaidia sekta ya elimu nchini, hivyo
kuibuwa chachu kwa wawekezaji wengine kusaidia sekta hiyo.
"Hii
ni sadakatul jariya kubwa sana nae Mungu atamfungulia biashara zake",
alisema.
Alisema
Said Bakhresa ni mwekezaji mzalendo ambae amekuwa mfano mzuri wa kuigwa katika
kuwekeza miradi mbali mbali ya maendeleo, hivyo kutoa fursa kadhaa za ajira kwa
vijana wa Kizanzibari.
Aidha,
aliwapongeza wananchi wa Bwefum kwa
kutoa ushirikiano mkubwa wakati ujenzi huo ukiendelea.
Vile
vile alimpongeza Dk. Shein kwa jitihada kubwa anazozichukuwa katika kusimamia
sekta ya elimu nchini na kubainisha kuwa hatua hiyo inatokana na kutambuwa
umuhimu wa elimu kuwa ndio msingi wa maendeleo.
Nae,
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Amali Dk. Idrisa Muslih Hijja akitoa
maelezo ya kitaalmu kuhusiana na ujenzi huo, alisema Skuli hiyo imejengwa kwa
mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya Union
Property Developers Ltd ya Tanzania.
Alisema
kazi ya ujenzi huo ulioanza Septemba mosi, mwaka 2016 na kumalizika Disemba 2,
2018 ukitekelezwa na Kampuni ya Quality
Building Contactors Ltd ya Zanzibar, kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni
2.4 hadi kukamilika kwake.
Alisema
mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ujenzi wa skuli hiyo ya
ghorofa moja ni kusamehe Kodi ya vifaa vyote vya ujenzi.
"Serikali
pia itakuwa na jukumu la kufanya matengenezo madogo madogo na kurekebisha
kasoro nyengine zitakazojitokeza, ikiwa ni hatua ya kuitunza skuli hiyo",
alisema.
Dk.
Idrisa alisema Wizara imepanga kuigawa skuli hiyo na kuwa skuli mbili, ikiwa ni
skuli ya Msingi Bwefum na Skuli ya Sekondari ya Bwefum, zitakazokuwa na utawala
tofauti kwa lengo la kusaidia uongozi katika usimamizi wa skuli hizo,
kuambatana na mfumo wa ugatuzi nchini.
Alitumia
fursa hiyo kuishukuru Kampuni ya Union Property Developers Ltd kwa uamuzi na
moyo wao wa kizalendo katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika dhana ya
kudumisha Mapinduzi.
Alitowa
wito kwa viongozi wa skuli, walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla, kuitunza na
kuienzi skuli hiyo ili iweze kutumiwa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.
No comments:
Post a Comment