Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Isack Kamwelwe akisisitiza jambo kwa mkandarasi Dott anayejenga
barabara ya Mtwara-Mlivata KM 50 mara baada ya kuikagua (kulia), kwake ni Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mtwara Mhandisi John Chacha na
kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw, Evod Mmanda.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Isack Kamwelwe kushoto na Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS
Mkoa wa Mtwara Mhandisi John Chacha wakikagua ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mlivata
KM 50 inayojengwa na kampuni ya Dott.
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amemtaka mkandarasi Makapo Contractors and General Supplies co. Ltd anayejenga barabara ya Masasi-Mpeta KM 16 na Dott Service Limited anayejenga barabara ya Mtwara- Mlivata KM 50 kukamilisha barabara hizo kwa wakati.
Amesema kuanzia sasa Serikali haitakuwa na muda wa
kumwongezea mkandarasi atakayebainika amechelewesha ujenzi kinyume cha mkataba.
“Nimeridhika
na ubora wa kazi yenu ni nzuri ila ongezeni kasi ili manufaa ya kuwepo kwa
barabara ya lami kwa wananchi wa Mtwara yalete matokeo chanya haraka”, amesema
Mhandisi Kamwelwe.
Amesema barabara ya Masasi-Mpeta KM 16 na Mtwara-
Mlivata KM 50 ni sehemu ya barabara kuu ya uchumi Mkoani Mtwara yenye urefu wa
KM 210 inayoanzia Mtwara mjini kupitia Mlivata, Nanyamba,Tandahimba, Newala hadi
Masasi.
“barabara
hii ikikamilika kwa wakati itaufungua uchumi wa wakazi wa Mtwara kwa kuongeza
fursa za ajira, kilimo na biashara”, amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.
Naye
mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw, Evod Mmanda ameishukuru serikali kwa kasi yake
katika ujenzi wa barabara hiyo ambayo ikikamilika itachochea utekelezaji wa
sera ya viwanda, utalii, kilimo na uvuvi
na hivyo kuzalisha fursa nyingi za ajira kwa wananchi.
“Tumejipanga
kuhakikisha tunashirikiana na mkandarasi
MAKAPO na DOTT ili kazi zao ziende kwa haraka na kuiwezesha Serikali kuendelea
kujenga barabara za lami katika maeneo ya Nanyamba,Tandahimba,Newala na hivyo
kuuunganisha kwa lami mkoa wa Mtwara na wilaya zake.
Waziri
wa Mhandisi Kamwelwe yuko mkoani Mtwara kukagua miradi ya ujenzi wa miundombinu
ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano na kuhimiza kasi ya ujenzi.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
No comments:
Post a Comment