TTCL TANZANIA YAZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA 2018 JIJINI DAR ES SALAAM - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 1 October 2018

TTCL TANZANIA YAZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA 2018 JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kulia), pamoja na Wakili Hamza Jabir kutoka Crax Law Partner (katikati), wakikata keki maalumu wakati  wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya huduma  kwa mteja 2018 ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ally Mbega.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kushoto), akitoa zawadi ya muda wa maongezi wenye thamani ya sh.5000 kwa wateja wa kwanza kufika duka la shirika lililopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kushoto), akipeana mkono na mmoja wa wateja baada ya kumpa zawadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kushoto), akipeana mkono na Ibrahimu Tini, mmoja wa wateja baada ya kumpa zawadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kushoto), akipeana mkono na mteja aliyemzawadia zawadi.


Wafanyakazi wa shirika hilo wakitoa huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (wa tatu kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo.

Wateja wakilishwa keki.


Wateja wakilishwa keki

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kujenga utamaduni wa kupenda vitu vya kwao jambo litakalosaidia kukuza pato la Taifa.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba wakati akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo wakati akifungua maadhimisho ya wiki ya huduma  kwa mteja 2018 Makao Makuu ya shirika hilo leo hii.

"Tunatoa wito kwa wananchi wote kuonesha uzalendo kwa kupenda vitu vya kwetu, kuunga mkono shirika letu la kizalendo kwa kutumia huduma zake ambapo ufanisi wa shirika letu utaongeza uwezo wa Serikali katika kuwahudumia wananchi kupitia mchango utakaotolewa na shirika hili katika pato la Taifa" alisema Kindamba.

Kindamba alisema katika wiki hiyo muhimu viongozi wakuu wa shirika hilo watawahudumia wateja katika maduka yao, watapokea maoni, kero na ushauri kutoka kwa wateja pamoja na kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali zitakazoripotiwa na wateja sanjari na kutoa zawadi lengo likiwa ni kuwashukuru wateja kwa ushirikiano wanaopata katika biashara.

Aliongeza kuwa shirika hilo ni mali ya watanzania kwa asilimia 100 na linafanya mengi kwa ajili ya watanzania na kuwa kila hatua wanayoichukua ina lengo kuongeza ufanisi wa huduma zao na kurahisisha maisha ya wananchi ambao ndio wateja wao wa kuu.

Alisema TTCL Corporation sasa ina jukumu mahsusi la kusimamia maendeleo ya sekta ya Mawasiliano kwa kuwaunganisha wananchi wote, kusimamia ufanisi wa miundombinu ya kimkakati ya mawasiliano kwa niaba ya serikali, kusaidia shughuli za ulinzi na usalama wa nchi, kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, huduma za jamii na ufanisi wa sekta nyingine zote.

Kindamba alisema tangu TTCL Mpya izaliwe wamefanya mambo mengi kama kuongeza kasi ya kuhudumia wateja, kubadili mwonekano na kuleta nembo mpya, maduka na vituo vya huduma kwa wateja vimeboreshwa na kuwa vya kisasa sanjari na kuingiza bidhaa mpya sokoni, kuanzisha kwa huduma za Fedha Mtandao pamoja na huduma zao kupatikana nchi nzima kama walivyojiwekea malengo.

No comments:

Post a Comment