Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka benki ya NMB, Omary Mtiga (kulia) akizungumza katika tukio hilo. |
NAIBU Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anastazia Mabula amezitaka taasisi za
fedha pamoja na waendelezaji milki binafsi kushirikiana na Serikali ili kutatua
changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba na makazi nchini.
Akihutubia
katika ufunguzi wa maonyesho ya nyumba yaliyoandaliwa na benki ya NMB jana na
kufanyika katika viwanja vya Kambarage jijini Dodoma, Mabula amesema serikali inauhaba
wa nyumba za watumishi hususani baada ya serikali kuhamia jijini Dodoma.
Amesemakuwa
Tanzania inaupungufu wa nyumba 3,000,000, hivyo ili kutatua changamoto hiyo,
kunatakiwa kujenga nyumba zaidi ya laki mbili kila mwaka
hivyo hawana budi kuwashirikisha wadau kikamilifu kama benki ya NMB ilikuziba pengo hilo.
Akizungumzia upande
wa Dodoma, Mabula amesema mahitaji ni kuwa na nyumba zaidi ya elfu 23
lakini zilizopo ni nyumba 1329 tuhivyo maonyesho hayo yaliyowakutanisha wateja wa
benki ya NMB, waendelezaji milki pamoja na wauzaji wa vifaa vya ujenzi
yana tija kubwa kwani yanalenga kuiunga mkono serikali katika suala la maendeleo.
“Makazi bora
ni haki ya kila mwananchi, na tukiri kuwa tuna changamoto ya uhaba wa nyumba
nchini, lakini kupitia maonyesho haya tunaweza kukutana na wadau mbalimbali
kama vile taasisi za fedha waendelezaji miliki na pia wauzaji wa vifaavya
ujenzi ili kumaliza changamoto hiyo,” Alisema Mabula.
Amesema
Serikali imeshaweka mazingira wezeshi yanayoruhusu taasisi za serikali pamoja
na waendelezaji milki binafsi kushiriki katika kuzalisha nyumba ambazo wananchi wanaweza kununua kupitia mikopo
inayotolewa na benki za biashara hivyo kuzitaka benki hizo kutoa mikopo kwa
riba nafuu ambayo hata mwananchi wa kipato cha chini ataweza kuimudu.
“Taasisi za
fedha ziangalie viwango vya riba, tusiwaumize wananchi, lakini kwa upande wa
wadau wengine naomba msogeze huduma zetu karibu na jamii, sambamba na kujenga
nyumba kwa kuzingatia mahitaji ya walaji, kuna wa chini, wa kati na wa juu,
wote muwape huduma kulingana na halizao,” Alisisita Waziri huyo.
Naye Meneja
wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi amesema lengo la maonyesho hayo ya sikumbili
ni kuwakutanisha wateja wa benki hiyo pamoja wadau mbalimbali wa nyumba ili kuweza
kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba na makazi iliyopo kwa sasa kwa kuzingatia
kuwa sekta hiyo inakuwa kwa kasi.
“NMB tumeona hii ni nafasi ya kuhakikisha tuna
uwezo wa kuwapa mikopo wateja lakini pia tuwalete karibu na wauzaji wabidhaa mbalimbali
kwenye sekta hii ili wateja waweze kuona na kulinganisha,…hii ni katika ushindani
wa kibiashara ili wateja waweze kupata kitu bora,” Alisema Mlozi.
Awali akimkaribisha
mgeni rasmi, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka benki ya NMB, Omary
Mtiga amewataka wateja wa benki hiyo kutumia fursa hiyo kwani wanatoa mikopo rahisi
na yenye masharti nafuu na muda wa kurejesha ni mrefu.
Amesema tayari
wameshatoa mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 13 nchi nzima, na kwa mkoa wa
Dodoma wametoa mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 700 na wanaendelea kutoa
mikopo hiyo ili kuiunga mkono serikali katika azma yakustawisha makao makuu ya
Serikali.
No comments:
Post a Comment