RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA KUMUAGA MAREHEMU ‘KING MAJUTO’ KATIKA KARIMJEE - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Thursday, 9 August 2018

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA KUMUAGA MAREHEMU ‘KING MAJUTO’ KATIKA KARIMJEE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Hamza Amri Athuman mtoto wa marehemu Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally akisoma dua kumuombea Marehemu Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mara baada ya dua hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliongoza mamia ya wananchi kutoa heshma za mwisho katika msiba huo. PICHA NA IKULU.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kufuatia kifo cha msanii mkongwe hapa nchini Mzee Amri Athuman maarufu kwa jina la King Majuto kilichotokea Agosti 08, 2018 Jijini Dar es Salaam.

King Majuto amefariki dunia majira ya saa 1:30 Jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo Mhe. Rais Magufuli amemtaka Dkt. Mwakyembe kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya Marehemu, Wasanii wote nchini, wadau wa sanaa, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha King Majuto.

Mhe. Rais Magufuli amesema King Majuto atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa na wa muda mrefu alioutoa kupitia sanaa ya uigizaji na uchekeshaji, ambapo alishiriki kuelimisha jamii, kuendeleza na kukuza sanaa na kuunga mkono juhudi za chama na Serikali katika kuhimiza maendeleo.

"King Majuto alikuwa kielelezo cha safari ndefu ya sanaa kwa nchi yetu, kwa muda wote amedhihirisha kipaji, ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika uigizaji na uchekeshaji na hivyo kuwa kipenzi cha Watanzania na wasanii wenzake, hatutasahau ucheshi wake, upendo na uzalendo kwa nchi yake wakati wote wa uhai wake" amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amesema anaungana na familia na wote walioguswa na kifo cha King Majuto katika kipindi hiki cha majonzi na amemuombea kwa Mwenyezi Mungu apumzike mahali pema peponi, Amina.

Inna lillahi wa inna ilaihi raji'un

No comments:

Post a Comment