| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea kiatu kwa naiba ya Namungo FC, kutoka kwa Mkurugenzi wa Haojue Brand Martin Francis, Wilayani Ruangwa, Agosti 10.2018 (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu). |
*Ni Uzinduzi wa uwanja
wa Halmashauri Ruangwa
HALMASHAURI ya Wilaya ya Ruangwa Agosti, 11, 2018 inatarajia
kuzindua uwanja wake wa michezo, ambapo timu ya wilaya hiyo Namungo FC
inayoshiriki ligi daraja la kwanza itapambana na bingwa wa ligi kuu 2018/2019
Simba SC ya jiji Dar es Salaam.
Timu hiyo ya Namungo
FC ambayo inamilikiwa na wachimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Namungo
wilayani Ruangwa ilianza 2009 kamasehemu ya mazoezi kwa wachimbaji hao mara
wanapotoka kazini, imeupa heshima mkoa wa Lindi kwa kuwa ndiyo pekee inayoshiriki
ligi daraja la kwanza.
Akizungumza wakati wa
ukaguzi wa uwanja huo leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018) Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa amesema mbali na timu ya Simba pia timu hiyo inatarajia kucheza na
timu za Yanga , Azam za jijini Dar es Salaam na Dodoma FC ya jijini Dodoma.
Uwanja wa mpira wa
miguu wa wilaya Ruangwa unaoitwa Majaliwa Stadium umejengwa katika kitongoji
cha Mtichi kata ya Nachingwea na ndio utakaokuwa unatumiwa na timu ya Namungo
FC kuchezea mechi za nyumbani.
“Lazima
tuisapoti timu yetu ya Namungo FC icheze daraja la kwanza kwa mafanikio
makubwa, hivyo ni vema tukashirikiana kuhakikisha timu hiyo inafanikiwa ili
ndoto ya kucheza ligi kuu itimie.”
Kadhalika Waziri Mkuu
amesema ni muhimu kwa timu ya Namungo FC kucheza na timu kama za Simba, Yanga,
Azam na Dodoma FC kwa sababu zinasaidia katika kuimarisha viwango vya wachezaji
na kuwaondolea uoga wa kupambana na timu nyingine.
Kiingilio katika mechi
ya Namungo FC na Simba SC ni sh. 3000. Tayari timu ya Simba imeshawasili
wilayani Ruangwa leo (Ijumaa, Agosti, 10, 2018), saa 11.01 jioni kwa ajili ya
mechi yake na timu ya Namungo.

No comments:
Post a Comment