JULIUS MTATIRO WA CUF AKIMBILIA CCM...! - THE HABARII

THE HABARII

HABARI | MATUKIO | MICHEZO.


ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 11 August 2018

JULIUS MTATIRO WA CUF AKIMBILIA CCM...!

Julius Mtatiro


MMOJA wa viongozi wa juu wa Chama cha upinzani nchini Tanzania, CUF Julius Mtatiro ametangaza kukihama chama hicho na sasa atajiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mtatiro anaingia katika kundi kubwa la baadhi ya viongozi toka vyama vya upinzani kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM, wengi wakiwamo wabunge na madiwani wakidai kumuunga mkono Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Pombe Magufuli.

Julius Sunday Mtatiro ni Mtanzania kijana aliyekuwa mpenzi na mwanachama wa CUF kwa takribani zaidi ya miaka 10 sasa huku akiwa vuma kwenye mitandao kwa kauli zake za kisiasa za mara kwa mara. Kauli ya kujivua CUF na kujiunga na CCM ameitoa leo na kuzua maswali kwa baadhi ya washabiki wake.

Mtatiro aliwahi kukamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa muda kwa tuhuma za kudaiwa kutuma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Facebook kumkashifu rais. Ujumbe huo wake ulidaiwa kumkashifu Rais Magufuli, hatua ilokuja kufuatia utekelezaji wa sharia ya kimitandao nchini. Katika tuhuma hizo; Mtatiro aliandika swali kwenye ukurasa wake wa facebook akiuliza ''Rais kitu gani bwana?'' jambo ambalo lilimsababishia kuingia matatani.

No comments:

Post a Comment