MAKALLA: CCM NDIYO YENYE DHAMANA YAKUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Saturday, 7 June 2025

MAKALLA: CCM NDIYO YENYE DHAMANA YAKUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

 Amemuelekeza waziri wa maji kufika Arumeru magharibi kutatua changamoto ya maji.

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema pamoja na mafanikio yaliyopo wanatambua kuwa kuna changamoto na CCM ndiyo wenye dhamana ya kutatua changamoto hizo na kupeleka maendeleo kwa watanzania.

Makalla ameeleza hayo leo Juni 6,2025 wakati akisalimia wananchi katika Jinbo la Arumeru Magharibi mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Arusha mjini kwa ajili ya mkutano wa hadhara akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Makalla ameeleza hayo alitaja utatuzi wa changamoto ya maji iliyopo katika eneo hilo akisisitiza Waziri wa Maji, Juma Aweso akitoka kushughulika na maji Karatu atafika Arumeru kuhakikisha pia wanapata maji ya uhakika.

“Kama kuna changamoto ya maji basi, Waziri wa Maji Juma Aweso atakapotoka Karatu aje katika kwenye Jimbo hili la Arumeru Magharibi aje ashirikiane nanyi muangalie utaratibu watu pana changamoto ya maji, nataka niwahakikishie changamoto za watanzania hakuna mbadala ni CCM itatachua changamoto hizo,” amesema Makalla.

No comments:

Post a Comment