UMEME WA REA WALETA NEEMA HOMBOLO DODOMA KATIKA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Monday, 29 July 2024

UMEME WA REA WALETA NEEMA HOMBOLO DODOMA KATIKA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA

BAADHI ya Wananchi kutoka katika Mitaa ya Kolimba na Hombolo Bwawani Kata ya Hombolo Halmashauri ya Jiji la Dodoma,wamesema uwepo wa Umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini(REA) umekuwa na Mchango na Mchango mkubwa katika uboreshaji wa huduma za  Afya.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti  baadhi ya wananchi  kutoka  Kata ya Hombolo Mkoani Dodoma wamesema  umeme wa REA umekuwa na tija kubwa katika maeneo yao hasa kwenye sekta ya afya.

“Umeme wa REA unasaidia sana hasa kuhifadhi dawa za Kinga kwa Watoto Wachanga pia umeme huu umerahisisha uwepo wa maji ya uhakika  pia kuwa na fursa ya  kila mtu kuwa na uwezo wa kuchemsha maji ya kunywa nyumbani kwa kutumia heater maana hapo mwanzo huwezi hata kuchemsha umeme w REA haukuwepo hivyo ilikuwa kila mtu anapata nafasi ya kuunganishiwa kwa bei ndogo tu na tunashukuru sana kwa kutukumbuka  “amesema Elizabeth Joseph.

Hii ni baada ya Wizara ya Afya,kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa  ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) katika kutekeleza mradi wa kupambana na Magonjwa ya Mlipuko ikiwemo Kipindupindu na Uviko-19 kusambaza umeme katika visima ambavyo havikuwa na pampu za umeme za kuvuta maji na vituo vya kutolea huduma za afya katika Mkoa wa Dodoma kwa Wilaya za Dodoma, Chamwino,Bahi, Chemba, Kongwa na Mpwapwa.

Mikoa mingine inayotekelezwa na Mradi huo ni Mwanza, Kagera, Simiyu, Kagera, Arusha, Pwani, Lindi, na Mtwara.

No comments:

Post a Comment