TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAHASIBU AFRIKA - THE HABARII

ASAS GROUP

Habari Mpya


Wednesday, 24 July 2024

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAHASIBU AFRIKA

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akiongoza Mkutano wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu  wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho cha AICC, ambapo Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA Leonard Mkude, Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu wa Afrika, ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase na Mkurugenzi Mkuu wa AICC, Bi. Christine Mwakatobe, wamewaeleza wanahabari kuwa mkutano huo unatarajia kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii pamoja na kuitangaza sekta ya utalii ya Tanzania, kwa wajumbe kutembelea vivutio vya utalii, hususan vilivyoko katika ukanda wa Kaskazini.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wahasibu Wakuu wa Afrika ambaye pia ni Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Lesotho, Bi. Malehlohonolo Mahase, akizungumza wakati wa Mkutano na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu  wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting) unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo amesema kuwa Mkutano huo utakawakutanisha pia Jumuiya za wafanyabiashara na watapa fursa ya kujua ni namna gani Afrika ipo tayari katika suala la uwekezaji na namna ya kuripoti hali ya Uchumi ya Afrika, jambo ambalo litaongeza uwazi na uwajibikaji.

Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Leonard Mkude, akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), kuhusu ujio wa Mkutano wa  Pili wa Kimataifa wa Wahasibu Wakuu  wa nchi za Afrika (African Association of Accountants General-AAG Meeting), unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Disemba Mwaka huu, katika Kituo hicho cha AICC, na utawashirikisha zaidi  ya washiriki 2,000 kutoka nchi za Afrika na mkutano huo unalenga kujenga Imani ya umma katika Mifumo ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwa Ukuaji Endelevu.

No comments:

Post a Comment